DULLY SYKES ATHIBITISHA KUWA HANA MAPOZI


Pamoja na kwamba wasanii wengi wapya kwa sasa ndio wanaongoza kwa kushutumiwa kuwa na na mapozi kwa watu wasiowafahamu Tanzania, Baba wa Bongo Fleva mwimbaji Dully Sykes amedai kuwa  hawezi kumuwekea pozi mtu yeyote kwa sababu ina madhara yake.

Dully amesema “Sauti yangu inafanya vizuri kutokana na watanzania, Mtanzania wa aina yeyote ni rafiki yangu nitamsaidia mtu yeyote nikiwa na kipato kama kuna uwezo, sibagui kabisa kabisa mimi ni rafiki wa kila mtu naongea na kila mtu”

Kuthibitisha kwamba anamaanisha anachokisema, Dully amesema hana tatizo kugawa mawasiliano yake kwa mashabiki, kuanzia kwenye bbm mpaka namba ya simu ambayo ameitenga maalum kwa ajili ya mashabiki zake

Posted by Bigie on 5:46 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.