FILIKUNJOMBE AMCHANA HADHARANI WAZIRI ANAYEONGOZA KUTAFUNA MALI ZA WATANZANIA


Kwenye video iliyopachikwa hapo chini, zingatia kuanzia dakika ya 2:57 na kwenye audio iliyopachikwa hapo, utamsikia mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akitamka na kufafanua yafuatayo:
  • Nchi yetu inatafunwa, na sote tunaona na Watanzania wanashuhudia.
  • Wanaofanya nchi yetu iangamie, wanaofanya ubadhirifu huu utokee, ni Mawaziri.
  • Sisi tuliopewa dhamana baadhi yetu siyo waaminifu.
  • Baadhi ya Mawaziri mnafanya maamuzi kwa maslahi binafsi.
  • Nchi hii siyo mali ya CCM, Tanzania ni mali ya Watanzania, sote.
  • Tunajua mnalindana, na huo ulinzi tunajua siyo bure, ingekuwa ni bure msingetoa nguvu za namna hii. Nchi inakufa, nyie mnalindana!
  • Nitamtaja Waziri mmoja, ambaye yeye anaongoza kwenye kutafuna mali za Watanzania. Waziri wetu wa Fedha si Mwaninifu. Waziri Mkullo si Mwaminifu! Aliyelidanganya bunge siyo Zitto Kabwe, aliyelidanganya Bunge ni Waziri wa Fedha.
  • Tunawasingizia watendaji wetu lakini ninyi Mawaziri ndiyo mmegeuka kuwa mchwa.
  • Waziri Mkuu, hatuna imani na baadhi ya Mawaziri wako!
  • Mfano wa mahali fedha zinakoliwa, ni kwenye fedha za Wanafunzi, mfano ni Mkuu wa Chuo cha Mkwawa. Wanafunzi masikini hawasomi, na wanapoandamana kudai haki yao, tunawapiga mabomu. Wanaopaswa kupigwa mabomu wamekaa wametulia maofisini. Aliyetafuna fedha ndiye aliyepaswa kupigwa mabomu. Yule Mkuu wa Chuo aliyetafuna fedha ya wanafunzi ndiye aliyepaswa kupigwa mabomu.
  • Jana mbunge mpya, Nassari amefika ana ripoti zote, lakini Waziri anasema hana ripoti.
  • Kama kuna kosa kubwa tunalolifanya, ni kudhani kuwa Tanzania ni mali ya CCM.


Posted by Bigie on 5:46 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.