KAMPUNI YA MAFUTA YA BP YAKUBALI KULIPA FIDIA

Kampuni ya mafuta ya BP imekubali kulipa fidia ya dola za kimarekani bilioni 7.8 kabla ya kesi kufika mahakamani kutokana na watu wanaoishitaki kampuni hiyo kwa sababu ya mafuta yaliyomwagika kutoka kisima cha mafuta cha BP katika ghuba ya Mexico miaka miwili iliyopita na kusababisha
 hasara za kiuchumi na mazingira kwa watu zaidi ya laki moja.

Watu kumi na moja walipoteza maisha huku mamilioni ya mapipa yakimwagika katika pwani ya Marekani baada ya bomba la mafuta kulipuka ambapo Wengi walioathirika ni wavuvi waliokosa kazi.

Bp imesema imetoa fidia lakini haimaanishi kwamba imefanya makosa katika kilichotokea ambapo sasa pia inakabiliwa na mashitaka kutoka serikali ya Marekani na wenye hisa ndani ya kampuni hiyo.

Posted by Bigie on 5:45 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.