Makato ya mshahara wangu PAYE, NSSF, GGM PF... INAUMA!
JAMII 5:42 AM
---------- MWANZO wa Forwarded message ----------
Angalia hiyo PAYE.
Sasa mimi ni mtu wa kawaida sana, kuna watu wanakatwa kodi milioni na kitu kila mwezi, halafu naona wagonjwa wanalala chini, wanafunzi wanakaa chini. Leo hii eti Mwanza kuna shule Pasiasi watoto wanakaa chini na hapo ni mjini, je huko Kayenze itakuwaje?
Inauma sana kama mimi kila mwezi nakatwa PAYE kubwa sana halafu wengine wanahujumu.
Inauma!
Watu wote kwa namna moja tunashiriki kujenga Taifa hili. Hivyo viongozi kumbukeni tunawachagua muongoze Taifa na sikuhujumu.
Haipendezi.
Ki uhalisia ingependeza sana kama tungeona kodi tunazokatwa zinafanyiwa kazi vizuri.
Sent from my BlackBerry® smartphone...

image via mabadilikotanzania@googlegroups.com
---------- MWISHO wa Forwarded message ----------
Ninatafakari...
Nimetizama hayo makato nikajiuliza maswali mengi na hivi ninavyoandika sijamaliza kujiuliza, kwa hivyo sitayaandika na wewe usijifanye hujui wala huoni tatizo na kwamba kila kitu kipo sawa. Unajua utakuwa unajiongopea!Nimewahi kuwaambia marafiki zangu na nitaendelea kuwaambia, kwamba sisi tulalamike tu kwenye egroups, eforums, blogu, tovuti, magazetini, tutoe maoni redion na kwenye runinga, tuyahamishie vijiweni, baa na kila tunakotaka, badala ya kuyahamishia kwenye kuwajibishana na kutaka majibu yanayoendana na maswali yetu.
Tuendelee kusubiri kuambiwa yale wanayotaka kutuambia, kisha tuwape kisogo hali tumepindisha shingo kisha tukanung'unikie pembeni.
Mtu mmoja alisema, "tutaendelea Yesu akirudi!" Nami natamani kurudi kwake kuwe kumekaribia, awe hapo kwenye kona, labda...