Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Atoa Salamu za Mwisho Kwa Mwili wa Marehemu Brigedia Jejerali Mstaafu Adam Mwakanjuki
JAMII 5:31 AM

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wameubeba Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki,na kuingia katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja leo,ambapo Viongozi mbali mbali na wananchi pamoja na ndugu na jamaa, watatoa salamu zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akitia saini kitabu cha kumbukumbu cha Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki,katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Manazi mmoja Mjini Unguja leo,marehemu atazikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akitoa salamu za mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki,katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Manazi mmoja Mjini Unguja leo,marehemu atazikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimpa pole mjane wa Marehemu Brigedia Jejerali mstaafu Ikupi Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu,katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilshi Mnazi mmoja Mjini Unguja leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapa pole jamaa na ndugu wa Marehemu Brigedia Jejerali mstaafu Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu,katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilshi Mnazi mmoja Mjini Unguja leo

Baadhi ya wananchi,Jamaa na ndugu wa Marehemu waliofika kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki,katika viwanja vya zamani Baraza la wawakilishi Mjini Unguja leo

Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar kutokea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.





