Mama Salma Kikwete atembelea Hospitali ya watoto wenye ugonjwa wa kansa nchini Brazil

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimtazama mtoto anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo ambayo inapokea wagonjwa 4000 kwa mwezi inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto kuendelea kuishi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Anna Julia Telles mwenye umri wa miezi mitatu anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa Marli Aparecide dos Santos mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto kuendelea kuishi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya bidhaa zinazouzwa na Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa kwa ajili ya kupata fedha za kuwasaidia watoto hao huku Afisa ubalozi wa Tanzania nchini Brazili Tabu Makata akimuangalia. Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza mfanyakazi wa Hospitali ya watoto waougua ugonjwa wa kansa akielezea jinsi hospitali hiyo pamoja na jamii inavyotoa huduma ya kujitolea kwa wagonjwa. Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya kansa

Posted by Bigie on 3:07 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.