News Alert: Katibu Mwenezi wa Vijana Wilaya ya Londigo (CCM) nae Ajiengua CCM


Baada ya aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya kujiengua chama hicho na kutangaza kujiunga na CHADEMA juzi, jana Katibu Mwenezi wa Vijana Wilaya ya Longido iliyoko Mkoani Arusha pia, Ndg Yohana Laizer nae ameamua kukihama chama chake cha CCM lakini  bado hajaweka wazi atajiunga na chama gani. 

Lakini taarifa zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Laizer kuungana na Millya ambae ameamua kujiunga na CHADEMA.

Taarifa hizo zinaeleza kua uamuzi wa Katibu huyo Mwenezi unatokana na madai yake ya kuchoshwa na viongozi wa CCM kuchanganya siasa na mila kiasi kwamba imefikia mahali wanawatishia Wamasai kutojiunga na vyama vya upinzani.

Blog hii imepokea taarifa hizi kutoka vyanzo vyake vya kuaminika, lakini bado inaendelea kufuatilia usahihi wake…..

Posted by Bigie on 4:10 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.