CCM Yazidi Kumeguka Arusha, Diwani wa Kata Sombetini Nae Atangaza Kujiengua CCM


Diwani wa Kata ya Sombetini ya Jijini Arusha, Mh A. Mawazo (CCM) ametangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoani Arusha, Ndg Samson Mwigamba, zinaeleza kuwa Mawazo ametangaza uamuzi wake huo leo asubuhi Mjini Dodoma.

Baadae alifanya mahojiano na Redio 5 ya Arusha na kueleza kuwa meamua kuachana na CCM kwasababu chama hicho kimeshapoteza muelekeo.

Amedai kuwa wananchi wake wanazo tarifa za uamuzi wake huo.
Hatua ya Diwani Mawazo kujiondoa CCM inakuja zikiwa zimepita siku mbili tu tangu aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, James Ole Millya kutangaza kujitoa CCM na Kujiunga na CHADEMA.

Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mtaa Themi, pia ndani ya Mji wa Arusha wanatarajiwa kurudisha kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA.

Halikadhalika kuna taarifa ambazo bado hazijawa dhahiri kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha nae yuko mbioni kukihama chama chake.

Posted by Bigie on 4:13 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.