PICHA ZA LULU: WATANZANIA TUWE NA MOYO WA HURUMA MAANA HAKUNA ALIYE MNYOOFU

Hiki Ndicho Jamii Inachotaka Kuona?





Nimehuzunishwa na picha za Mahakamani kwenye magazeti ya jana zikimwonyesha msichana Elizabeth ' Lulu' Michael akilia  hadharani.

Nikivaa miwani ya mzazi nilimwona mtoto ambaye angeweza kuwa wangu. Nilimwona mtoto anayedhalilishwa mbele ya macho ya jamii. Nilimwona mtoto  anayehukumiwa na jamii ambayo hadi sasa haijui ukweli wa kilichotokea.

Jamii inapaswa kujiuliza, kwani picha za Lulu akiwa analia zina umuhimu kwa wanajamii kuziona?Je, ni kwa sababu machozi ya Lulu ni dhahabu kwa wengine? Kwamba yanasaidia kwenye kuuza magazeti? Je, kuwa na huzuni na kutoa machozi si haki ya hisia za mwanadamu ambazo zinapaswa kuheshimiwa? Kwa nini ziwekwe hadharani? Hicho ndicho jamii inataka kukiona? Na ikishaona?

Tutafakari.

Posted by Bigie on 10:47 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.