WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MWENYE DHAMANA YA MUUNGANO, MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA OFISI ZA CLOUDS MEDIA GROUP

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mwenye Dhamana ya Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mahojiano na Clouds Fm 88.4 Dar es Salaam kuelezea mambo machache yanayohusu Muungano. 
 
Pia ujio wake ndani ya Clouds Fm ni kuelezea changamoto zinazokabili Tanzania Bara na Visiwani inapotimiza miaka 48 tokea nchi hizi mbili zimeungana, changamoto ya kwanza ambayo Waziri amezungumzia ni ile ya mfanyabiashara kununua bidhaa Zanzibar wakija huku Tanzania Bara TRA nao wanatoza tena kodi, kama kwamba ametoka nchini nyingine.
 
 Suala lingine ni gawio la BOT kupata 4.5% ya gawio zima. Mengi zaidi unaweza kusikiliza Jahazi la Clouds FM na vipindi vingine vyote.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mwenye Dhamana ya Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na muandaaji wa Jahazi la Clouds Fm, Simalenga Simon

Posted by Bigie on 10:47 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.