TETESI ZA KUJIUZULU KWA MAWAZIRI KADHAA TANZANIA


Ni taarifa zinazosambaa katika mitandao jamii ya Facebook, Twitter kwenye eGroups na eForums. Taarifa hizi zinatofautiana na kwa kuwa hazijathibitishwa kwa namna yoyote ile, zitabaki kuwa TETESI tu. Ikiwa ni kweli itafahamishwa hivyo, ikiwa ni uongo, basi na tetesi hii ipuuzwe!

Unaweza kufuatilia mwenyewe kwenye ukurasa za Twitter zenye tweets za Watanzania, JamiiForums, MabadilikoTanzania na Wanabidii.

Mojawapo inasema: "Wanaotajwa kujiuzulu ni Mkulo-Fedha, Dkt. Chami - Viwanda na Biashara, Dkt. Mponda - Afya na Nungu - Uchukuzi. Inasemekana watatoa tamko usiku wa leo."
Breaking News ya Radio One, inasemekana mawaziri 8 wamejiuzulu..
— Joseph Msendo (@msendo4life) April 20, 2012
Nyingine inasema: 
 " Mawaziri hao ni; 
Waziri wa Fedha, 
Mustafa Mkulo, 
Waziri wa Viwanda na Biashara, 
Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, 
William Ngeleja, 
Waziri wa Uchukuzi, 
Omar Nundu, 
Waziri wa Maliasili na Utalii, 
Ezekiel Maige, 
Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, 
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
George Mkuchika, 
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na
 Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

Posted by Bigie on 1:14 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.