UJUMBE MAALUMU WAKUIKUMBUSHA FAMILIA KUTUMIA CHANDARUA WAZINDULIWA


Mabalozi wa Malaria hapa nchini sambamba na waratibu wa hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye hotel ya Serena,jijini Dar,hafla hiyo ilihusu uzinduzi wa ujumbe maalum ( Night watch)wa kuwakumbusha/kuikumbusha familia kutumia chandarua wakati wa kulala.
Pichani ni Dr Ally Mohamed ambaye ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini (NMCP),akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa ujumbe maalum ( Night watch)wa kuwakumbusha/kuikumbusha familia kutumia chandarua wakati wa kulala.
Mabalozi wa Malaria nchini wakiwa sambamba na wageni waalikwa na waratibu kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo .

Mmoja wa Mabalozi wa Malaria hapa nchini,Msanii Mwasiti Almas akimkabidhi  Muwakilishi wa kampuni ya Exxon Mobil,Michael Finlay,fulana yenye ujumbe wa mradi wa Malaria ZINDUKA,ikiwa ni sehemu ya hamasisho kwa jamii kupapambana ugonjwa huo ambao umekuwa ukisababisha vifo vingi kwa watoto.
Vijana wenye vipaji kutoka THT wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri mbele ya jukwaa 
Wageni rasmi katika uzinduzi huo wa ujumbe maalum ( Night watch) wa kuwakumbusha/kuikumbusha familia kutumia chandarua wakati wa kulala.
Mmoja wa Mabalozi wa Malaria nchini,Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Mwasiti akihojiwa kuhusiana na uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa ndani ya hoteli ya Serena jijini Dar.
Wageni waalikwa mbalimbali wakisalimiana na kubadilishana mawazo ya hapa na pale kabla ya uzinduzi rasmi.
Wageni waalikwa wakisalimiana kabla ya uzinduzi kufanyika
Picha mbalimbali za kumbukumbu kwa wageni waalikwa
Pichani kulia ni Dr Ally Mohamed ambaye ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini (NMCP),akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa ujumbe maalum ( Night watch)wa kuwakumbusha/kuikumbusha familia kutumia chandarua wakati wa kulala.
Burudani ya igizo la Malaria likitolewa na vijana wa THT kwa wageni waalikwa (hawapo pichani).
Mmoja wa waratibu wa uzinduzi  wa ujumbe maalum ( Night watch)wa kuwakumbusha/kuikumbusha familia kutumia chandarua wakati wa kulala kupambana na ugonjwa wa Malaria,Mama Sadaka Gandi akiwakaribisha wageni waalikwa sambamba na mgeni rasmi wa tukio hilo.
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo
Wageni waalikwa wakiwa makini kufuatilia uzinduzi huo.
Sehemu ya mabalozi wa Malaria na wageni waalikwa wakifuatilia jambo mbele ya jukwaa.

Mgeni rasmi,Dr Ally Mohamed ambaye ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini  (NMCP),akizungumza jambo na Mama Sadaka Gandi
Baadhi ya Mabalozi wa Malaria nchini,kutoka shotoni ni Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Amin,Barnabas,Mwasiti, Hamis Mandi a.k.a B Dozen (Mtangazaji Clouds FM),Fid Q waliohudhuria uzinduzi huo wa ujumbe maalum,kukuikumbusha familia kutumia chandarua wakati wa kulala,onaofanywa na Mabalozi wa Malaria (NIGHT WATCH) wa mradi wa ZINDUKA.

Posted by Bigie on 1:02 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.