FLORA MVUNGI ATIWA MBARONI
JAMII 12:13 AM
STAA sexy wa filamu za Kibongo, Flora Festo Mvungi ametiwa mbaroni kwa utapeli baada ya kudaiwa kuchikichia mshiko kutoka kwa muandaji wa muvi, Othmani Abdallah Nzwala aliyemfungulia kesi katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe jijini Dar.
Awali, mpekuzi wetu alipenyezewa habari kuwa, staa huyo anayewakilisha Kundi la 2gether alikubaliana na Othmani kuwa atashiriki filamu yake inayoitwa Mziwanda lakini muda ulipofika, Flora hakuonekana ‘lokesheni’.
“Alikuwa akinisikilizisha muziki kila nilipompigia simu hadi nikalazimika kumchezesha mtu mwingine katika zile scenes (vipande) alizopaswa kucheza Flora.
Kiukweli amepotezea gharama zangu nyingi na nimeamua kumfungulia jalada la kesi namba RB/ CHA/RB/3411/2012-UTAPELI,” alisema Othmani huku akikataa katakata kutaja kiasi cha fedha alichompa Flora.
Ili kupata mzani wa habari hiyo, mpekuzi wetu alimtafuta Flora kwa njia ya simu ya mkononi na alipopatikana alisomewa tuhuma zake, akafunguka:
“Hao ni wazushi, nilifika siku ya kwanza waliyoniita, lakini kamera yao ilikuwa inazingua sasa walipokuwa wananitafuta tena mimi nilikuwa sipo nikawaambia wanisubiri nirudi nitafanya kazi yao.”
Ishu hiyo bado ipo polisi ambapo muda wowote itasukumwa mahakamani.






