WANAFUNZI CHUO CHA MKWAWA IRINGA WAZIBA BARABARA -LIVE ENEO LA TUKIO
JAMII 7:50 AM
Wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa hivi sasa wameziba barabara kuu ya Iringa -Pawaga barabara inayosimamiwa na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) wakishinikiza kuwekwa matuta katika eneo la lango kuu la chuo hicho cha Mkwawa kutokana na ajali za mara kwa mara .
Wanafunzi hao zaidi ya 200 wameziba barabara hiyo eneo la Kuingia chuoni huku wakimtaka diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thobias Kikula .a.k.a MC Kikulacho kushirikiana nao kuibomoa barabara hiyo ili kuweka matuta kuanzia sasa.
Wakizungumza kwa jazba mbele ya diwani huyo wanafunzi hao wamesema kuwa wamelazimika kuziba barabara hiyo baada ya kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara kwa wanafunzi wanaovuka barabara hiyo kugongwa kutokana na madereva kuendesha magari yao kwa mwendo mkali zaidi.
Hivyo kutokana na ajali hizo wamemtaka diwani huyo kuungana nao katika kuchimba barabara hiyo ya lami ili kuweka matuta kuanzia sasa zoezi ambalo limekuwa gumu kwa diwani Kikulacho kuungana kulitekeleza .
Akijaribu kuwatuliza jazba wanafunzi hao bila mafanikio diwani Kikulacho alisema kuwa anaomba kupewa muda ili suala hilo aweze kulifikisha kwa wahusika kwa maana ofisi ya Tanroads mkoa na baraza la madiwani.
Hadi sasa hali ni tete na diwani bado amezungukwa na wanafunzi hao ambao wanaimba nyimbo za kama si juhudi zetu wenyewe diwani ungefikaje leo hapo huku polisi wakionyesha kuvuta subira kuwatawanya





