Washindi watatu kuwasindikiza nyota wa muziki wa tuzo za kili muzik awards 2012
JAMII 3:17 AM
Majaji wa kusaka vipaji vipya vya Ziara ya washindi wa Kili Awards 2012 mkoani Dodoma, Joseph Haule, Henry Mdimu, Queen Darleen na Juma Nature.
Mpambano unaendelea ambapo mpaka jioni hii watapatikana washindi watatu ambao watauwakilisha mkoa wa Dodoma katika Tamasha la washindi wa tuzo za Kilimanjaro za msimu huu litakalofanyika Jumamosi hii.
Wengine walikuja na vyombo vya ala, huyu akisaidiwa na muongozaji wa kipindi kupata muziki mzuri mbele ya majaji ambao hawapo pichani pia
Wasanii wanaochipukia kutoka mkoani Dodoma waliojitokeza katika ukumbi wa Club 84 katika usaili wa kuwa kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la ziara ya washindi itakayofanyika mkoani humo Jumamosi ya tarehe28 mwezi huu katika viwanja vya Jamhuri.





