UPDATE MPYA: TASWIRA ZA LULU MICHAEL ALIPOTINGA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU LEO

Mshatkiwa Elizabeth Michael |(17), ' Lulu'  akielekea kupanda ngazi na kupandishwa Kizimbani.
 Kesi hiyo  ilikuja kwa ajili ya kutajwa maana  Upelelezi haujakamilika. 
Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rita Tarimo kuwa upelezi bado haujakamilika,  hivyo kesi hiyo  itatajwa tena Mei 7 mwaka huu. Mtuhumiwa amerudishwa rumande.
 Akizindikizwa ndani ya chumba cha Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo
Mshtakiwa akipanda ngazi kuelekea Kizimbani ambalo kesi yake ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam huku akiwa katika ulinzi mkali kutoka kwa askari  Magereza.


Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiongozwa na Askari Magereza kuingia ndani ya gari baada ya kutajwa kwa kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo.

Lulu (katikati) akilindwa na askari lukuki


Lulu akiingizwa rokapu ya Mahakama ya Kisutu


Lulu akiwa ndani ya basi la Magereza tayari kupelekwa gereza la Segerea


Askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakilinda msafara wa mahabusi akiwemo Lulu

 

Kamishna wa tume ya haki za binadam, Joaquine De – Mello leo amejitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiambatana na mawakili wengine wa kujitegemea kumtetea msanii ya sinema, Elizabeth Michael aka Lulu.


Akilitaja jopo la mawakili wanaomtetea Lulu, wakili wa kujitegemea Kennedy Fungamtama, alisema kuwa mama De Mello ni miongoni mwa mawakili pamoja na Furgence Masawe na Peter Kibatala. Hata hivyo hawakuongea lolote mahakamani.


Wakili wa serikali
Elizabeth Kaganda alidai kuwa kesi imekuja kutajwa. Hata hivyo, alisema, upelelezi bado haujakamilika na kwamba anaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Ikapangwa kutajwa tena Mei 7, 2012.

Awali hali ilikuwa mshike mshike kumpitisha Lulu kutoka chumba cha mahabusu kumleta chumba cha mahakama kwa sababu watu walikuwa wengi pamoja na wanahabari waliokuwa wakimuwinda kupata picha yake. 


Korido ilikuwa ndogo kutokana na msongamano wa watu. Lulu alipitishwa akiwa amezungukwa na maaskari magereza bila shaka kuzuia asiguswe na watu au kumfanya jambo lolote.


Baada ya purukushani hiyo , aliingizwa mahakamani akilia kwa sauti kutokana na usumbufu alioupata kutokana na mbanano uliokuwepo, jambo lililolazimisha mlango wa chumba cha mahakama kufungwa na watu kusukumwa nje. 


Ikamlazimu Hakimu kutoa amri kuwa kesi hiyo iwe inasomwa mapema zaidi na kuwaamuru maaskari kuwaondoa watu wote ndipo atolewe kurudishwa mahabusu bila usumbufu tena. Alimpa pole Lulu kwa usumbufu alioupata.


Baada ya kutoka Kortini Lulu aliyekuwa amejitanda ushungi, alipelekwa kwenye gari na kuondolewa kwa kasi eneo la mahakama hiyo kwa basi la magereza, akiwa mfungwa pekee kwenye gari ile iliyojaa pia askari magereza waliokuwa wakimlinda.
******************************

HIZI NI PICHA ZAIDI TOKA GLOBAL PUBLISHERS 


Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa chini ya ulinzi mkali.
Lulu akiwa kawekwa mtu kati.
...Akitolewa mahakamani.

Askari wakidumisha ulinzi nje ya mahakama.
...Wakiwa na silaha zao tayari kwa lolote.

...Askari huyu akiandaa njia kabla ya Lulu kupitishwa.
Karandinga lililomleta Lulu mahakamani leo.
Baba mzazi wa Lulu nae alikuwepo mahakamani hapo.

Posted by Bigie on 2:35 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.