Watumishi wa Wizara ya Afya wapandishwa kizimbani kwa wizi
JAMII 4:22 AM
Pia, wanashtakiwa kwa kula njama, kutumia vibaya madaraka na kushawishi kutenda kosa kinyume cha tararibu za matumizi ya fedha za umma.
Washtakiwa hao ni Mkuu wa Chuo cha Afya ya Jamii na Uuguzi kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Veronica Mpazi, Makamu mkuu wa chuo, Laurentia Nkulila, Mhasibu wa chuo hicho, Philemon Orungi na mtumishi wa hazina ndogo, Atusubisye Mwabulambo.
Kesi hiyo ilitajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro na kuendeshwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU, Diana Madete na Debora Mlowe.
Mlowe alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya Aprili na Julai, 2009 saa za kazi kwenye chuo hicho.
Katika shitaka la kwanza, Mpazi, Orungi na Nkulila wanadaiwa kubadilisha matumizi ya Sh3,630,000 ambazo zilikuwa za chakula cha wanafunzi na kuzitumia kulipa posho za kufundisha masomo ya ziada na fedha za kujikimu kinyume cha taratibu za matumizi ya fedha hizo.
Shitaka la pili, washitakiwa wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuidhinisha na kusaini vocha za malipo mbalimbali kinyume cha sheria kifungu namba 85(2) na namba 87(1)g ya mwaka 2001 cha taratibu za matumizi ya fedha za umma.
Mwendesha mashitaka alizitaja vocha hizo kuwa ni zenye namba 1472 iliyoidhinisha Sh 633,630, namba 1473 ya Sh955,000, namba 1475 ya Sh1 milioni na namba 1474 ya Sh 675,000, fedha hizo ambazo ni mali ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Shitaka la tatu linalowahusisha washtiakiwa hao pamoja na mtumishi wa hazina ndogo, Mwabulambo, inadaiwa kwa pamoja walikula njama kuidhinisha fedha hizo na kubadili matumizi tofauti na taratibu za matumizi ya fedha za umma.
Mlowe aliendelea kudai kuwa shtaka la nne linamhusu Mwabulambo peke yake, kwa kusaidia kutendeka kwa makosa hayo yote huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Baada ya kusomewa mashtaka yote kwa pamoja, washtakiwa hao walikana kuhusika na kesi iliahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu itakapotajwa tena.
Hata hivyo, dhamana kwa washtakiwa ilikuwa wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mshtakiwa na Sh2 milioni za maandishi kila mdhamini, Methew na Orungi walishindwa kutimiza mashar





