WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA APEWA MASAA 72 YA KUJIUZULU
JAMII 10:23 AM
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Mh Zitto Kabwe amelitaarifu Bunge kuwa mchakato unaandaliwa kukusanya saini za wabunge 70 ili kuweza kupeleka hoja ya kulitaka Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Zitto amesema saini hizo 70 zinahitajika zwe zimepatikana kabla ya Jumatatu ( MASAA 72) ili kuwezesha uwezeshaji wa kuwasilisha hoja hiyo ili Bunge limlazimishe Waziri Mkuu kujiuzulu au vinginevyo mawaziri wote waliotajwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wawe wamejiuzulu badala yake.
Hii imetokea jioni hii Bungeni Dodoma ambapo wabunge wengi bila kujali itikadi za vyama vyao wameonekana kukerwa na utendaji mbovu wa mawaziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.





