WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAISI AFIKISHWA MAHAKANI KWA KWA UFISADI WA MILLION 74



Aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Arcado Ntagazwa (65), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kujipatia mali ya fedha za Kitanzania shilingi milioni 74 kwa njia ya udanganyifu.


Katika kesi hiyo iliyosomwa mahakamani hapo jana, Ntagazwa anashitakiwa pamoja na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wake, Dkt. Webhale Ntagazwa (29) na Seneta Julius Miselya (60).


Baada ya kusomewa mashitaka na kuyakana, waliachiwa kwa dhamana isipokuwa Miselya ambaye hakuwa ametimiza masharti ya dhamana kwa wakati huo.


Wakisomewa mashitaka yao jana mbele ya Hakimu Liud Chamshama, Mwendesha Mashitaka Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya alidai kuwa Ntagazwa na wenzake hao walijipatia mali hiyo kwa udanganyifu.


Baada ya kusomewa mashitaka na kuyakana, waliachiwa kwa dhamana isipokuwa Miselya ambaye hakuwa ametimiza masharti ya dhamana kwa wakati huo.


Wakisomewa mashitaka yao jana mbele ya Hakimu Liud Chamshama, Mwendesha Mashitaka Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya alidai kuwa Ntagazwa na wenzake hao walijipatia mali hiyo kwa udanganyifu.


Walidaiwa kuwa Oktoba 22, 2009 maeneo ya Mikoroshini Msasani katika Wilaya ya Kinondoni, washitakiwa kwa nia ya udanganyifu walijipatia kofia 5,000 na fulana 5,000 kutoka kwa Noel Severe zenye thamani ya Sh milioni 74.


Ilidaiwa na Komanya kuwa washitakiwa hao walimdanganya Severe kuwa bidhaa hizo wangezilipa baada ya mwezi mmoja tangu kupewa mzigo huo, jambo ambalo hawakulitekeleza. 
(via gazeti la HabariLeo)

Kesi ya "Lulu"

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayetuhumiwa katika kifo cha Steven Kanumba amefikishwa tena mahakamani na gari la Polisi aina ya Toyota Hiace akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wakimlinda dhidi ya kundi la waandishi wa habari, wapiga picha na raia waliofurika katika Mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo ya mauaji inayomkabili.



Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Rita Tarimo aliridhia maombi ya Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliyeiomba Mahakama kuondoa watu wote kwa hofu ya kusababisha vurugu mahakamani hapo.


Kamishna Haki za Binadamu amtetea Wakili wa kujitegemea, Kennedy Fungamtama, ambaye  anamtetea “Lulu”, aliwatambulisha mawakili wenzake wa utetezi katika kesi hiyo akiwemo Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu, Joaquine De-Mello, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.


Kaganda alidai kuwa kesi ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.


Aliiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutaja na ikapangwa Mei 7. Lulu anadaiwa kumwua msanii mwenzake, Kanumba Aprili 7, Sinza Vatican, Dar es Salaam. Yuko mahabusu kwa sababu kesi ya mauaji haina dhamana. (via gazeti la HabariLeo)

Posted by Bigie on 10:38 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.