BASI LA NBS LAUA WATU 7 NA KUJERUHI 54

.
.
.
WATU saba wamekufa na wengine 54 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya basi iliyotokea jana wilayani Igunga, Tabora.Habari zilisema ajali hiyo iliyohusisha basi la Kampuni ya NBS ilitokana na kupasuka kwa tairi moja la mbele na hivyo kusababisha gari kupinduka.

Kwa mujibu wa baadhi ya watu walioshuhuda, ajali hiyo ilitokea jana asubuhi mjini Igunga wakati basi hilo likitoka Tabora kwenda Dar es Salaam.Walisema maiti na majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Mganga mfawidhi  wa hiyo, Dk Godfrey Kissila, alithibitisha kupokelewa na kuhifadhiwa kwa maiti za watu waliokufa katika tukio hilo."Maiti hao ni za wanawake watatu, wanaume watatu na mtoto mmoja," alisema mganga huyo.

Alisema majeruhi wapatao 54 wamelazwa katika hospitali hiyo na kwamba saba miongoni mwao hali zao ni mbaya.Mara baada ya ajali hiyo, magari ya maalumu ya kubebea wagonjwa, yalikwenda katika eneo la tukio na kufanyakazi ya kubeba majeruhi na kuwapeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Katika hospitali hiyo, waganga na wauguzi walionekana wakishirikiana kujaribu kuokoa maisha ya majeruhi

Hata hivyo hadi wakati tunakwenda mitamboni, majina ya maiti na majeruhi yalikuwa hayajapatikana.

Akizungumuza na waandishi wa Habari Kamanda wa polisi mkoani Tabora Antony Lutta amesema kuwa ajari hiyo ilitokea majira ya saa nne asubuhi katika eneo hilo na kusababisha majeruhi 54 huku majeruhi kumi na mbili wakipata luhusa.

Kamanda lutta alisema kuwa chanzo cha ajari hiyo ni kupasuka kwa matairi ya mbele mpaka kusababisha gari hilo kukosa mwelekeo na kugonga mti aliongeza kuwa gari hilo lilizunguka mara mbili.

Alisema chanzo cha ajali hiyo taarifa za awali zinasema ni tairi ya mbele kupasuka,lakini bado uchunguzi wa kifo hifo hicho unafanyika na
taarifa rasmi itatolewa.

Kwanyakati tofauti majeruhi hao wakizungumuza na vyombo vya habari kwanyakati tofauti walisema kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi ambao ulisababisha kupasuka kwa matairi hayo.

Joseph Kisala Mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Igunga alisema kuwa watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo ni watu saba ambapo miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ya wilaya.

Aliongeza kuwa miili iliyo tambuliwa ni miwili kuwa ni Anna Kisima,Dicksono Nassani pamoja na Zainabu hamudu.

Kisima aliongeza kuwa majeruhi watano wanatarajiwa kupelekwa katika hospitali ya lufaa bugando mwanza kwa matibabu zaidi kulingana uhaba wa vifaa vya matibabu vya haospitali ya wailya ya Igunga.

Aliwataja majeruhi hao wanao tarajiwa kupelekwa hospitali ya Rufaa Bugando kuwa ni pamoja na Iddi Hussein ambaye ni dereva (34),kasongo athumani (36) na majeruhi watatu majina yao hayakuweza kupatikana.

Kamnda lutta alisema kuwa ulinzi wa mizigo ya majeruhi umethibitiwa vizuri pamoja na usalama wao kwa ujumla,

Aliongeza kuwa madereva wa magari ya abiri kabla hawajaondoka wakague magari yao sambamba na kuendesha kwa mwendo wa wastani kuzingatia arama za barabara.

Posted by Bigie on 7:04 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.