BREAKING NEWSSS: MBUNGE WA SEGEREA DR. MAKONGORO MAHANGA ASHINDA KESI ( RIPOTI KAMILI)

Dk. Milton Makongoro Mahanga

Mbunge wa Segerea, Dkt. Makongoro Mahanga (CCM) amekitetea vyema kiti chake cha Ubunge wa Segerea, Dar es Salaam kwa kushinda kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Fred Mpendazoe (CHADEMA) iliyokuwa inapinga ushindi uliopatikana katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010.

Mpendazoe anapaswa kulipa gharama zote za kesi.

Kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010 iliyosomwa leo na Jaji Profesa Ibrahimu Juma ambaye amekuwa akiisikiliza tangu ilipofunguliwa Novemba 10, 2010, ilikuwa ikipinga ushindi wa Mahanga kwa madai kuwa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi zilikiukwa katika hatua ya kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo.

Kutokana na dosari hizo, Mpendazoe ambaye alikuwa akiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala, aliiomba Mahakama itengue matokeo hayo na iamuru uitishwe uchaguzi mwingine mdogo katika jimbo hilo au imtangaze yeye kuwa mshindi akidai kwamba alipata jumla ya kura 56,962 na Mahanga kura 44,904.

Mbali na Dkt Mahanga ambaye alikuwa mdaiwa wa pili katika kesi hiyo, mdaiwa wa kwanza alikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wa tatu alikuwa ni Msimamizi wa Uchaguzi (RO), katika jimbo hilo.

Dkt. Mahanga alikuwa akitetewa na Mawakili Jerome Msemwa na Aliko Mwamanenge na AG na RO wamekuwa wakitetewa na Mawakili wa Serikali, David Kakwaya na Seth Mkemwa.

Wakati wa ushahidi wake, upande wa madai uliwaita mahakamani mashahidi 13 akiwemo mlalamikaji mwenyewe Mpendazoe na wadaiwa wote watatu kwa pamoja waliwaita jumla ya mashahidi 16.

Posted by Bigie on 3:39 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.