WOLPER AJIGAMBA: "UWOYA HANIWEZI"...


 

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper (pichani) ameibuka na kumtambia mnyange anayetesa katika kiwanda hicho, Irene Uwoya akisema: “Uwoya haniwezi. Hakuna mtu anaweza kunitishia maisha.”

Akizungumza na mpekuzi wetu hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Wolper alisema tangu amezaliwa hajawahi kupigwa hata na wazazi wake hivyo itakuwa jambo la aibu sana kwake kupigwa ukubwani.

“Hakuna mtu anayeweza kunifanyia lolote, mimi ninajiamini kuliko kawaida. Simuogopi mtu yeyote wala sihofii chochote kwa sababu sijamfanyia mtu ubaya wowote,” alisema Wolper na kuongeza:

“Kama Uwoya anaona nimekosea kweli na adhabu yangu ni kipigo, aje anipige, ingawa ninauhakika hawezi kufanya hivyo. Hapa amefika.”

KWA NINI YOTE HAYA?
Hivi karibuni gazeti la Risasi Jumamosi liliripoti habari yenye kichwa kisemacho; ‘Msiba wa Kanumba… Uwoya: Lazima nimpige Wolper’.

Katika habari hiyo, Uwoya alieleza sababu tatu za kumpiga Wolper ikiwemo ile ya kusafiri na kuacha maziko ya marehemu Steven Kanumba yakiendelea wakati alikuwa ni mtu wa karibu sana na msanii huyo.

Posted by Bigie on 3:33 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.