KUMEKUCHA SHINDANO LA MISS EAST AFRICA 2012

Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wameanza kutangazwa.
Rahwa Afeworki

Mrembo wa kwanza kupatikana ni Miss Rahwa Afework (22) kutoka Nchini Eritrea ambae aliwashinda wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Eritrea katika mashindano hayo.

Miss Rahwa Afework mwenye urefu wa 1.73m anasomea mambo ya Fashion design Nchini Eritrea.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam .

Posted by Bigie on 11:08 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.