MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA

 Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika hapa nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.

Na Ally Rashid Dilunga
Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na ambaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard

Aidha Mheshimiwa Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Rais wa Benin. 

Balozi Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara letu la Afrika.

kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama Joan Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa nchini Uingereza. Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.
 Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
 Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George, maarufu kama Queen wa Blog hapa Uingereza.
 Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
 Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika jijini  London

Posted by Bigie on 7:52 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.