BREAKING NEWZZZZZZZ........ VURUGU KUBWA YAZUKA ZANZIBAR USIKU HUU
habari za kitaifa 7:57 PM

TAARIFA ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE TOKA VISIWANNI ZANZIBAR,INAELEZA KUWA KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LIMEVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO USIKU HUU NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA LEO KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO.
WAPEKUZI WETU WANAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HIZI ,HIVYO TUVUTE SIBIRA KWA SASA.
