Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika kumaliza mkutano wao leo nchini afrika kusini
habari za kitaifa 6:07 PM

Pichani shoto ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,jana jioni,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya kumbi ya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini.Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na mwisho ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo.

Pichani kulia ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo akifafanua jambo kwa makini wakati wa mchakato wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ulipokuwa umepamba moto jioni ya leo,katika mkutano uliofanyika kweny moja ya kumbi ya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini jana mchana,Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa

Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo.

Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo


Pichani juu na chini Mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ukiendelea ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini jana mchana.

Baadhi ya Marais Wastaafu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,ambaye pia ni Mratibu mkuu wa mkutano huo wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Mkutano huo jana mchana.

Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin,Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar,Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Rais Thambo Mbeki wa Afrika Kusini,Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria,Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Rais Rupiah Banda wa Zambia wakiwa katika picha ya pamoja jana mchana kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akijadiliana jambo na Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin walipokuwa wakiwasili kwenye viunga vya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini jana kwa ajili ya kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
![]() |
Pichani mbele ni Marais Wastaafu wa Tanzania,Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Amani Abeid Karume sambamba na Marais wengine wakiwasili katika viwanja vya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika. |

Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka nchini Tanzania,wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kuripoti mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.Shoto ni Yvonne Msemembo (ITV) ,Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper),Nestor Mapund,Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications), Muondosha Mfanga (The Guardian) pamoja na Deus Mjatta (ITV).

Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya ukumbi,kabla ya kuanza kwa Mkutano huo,Shoto ni Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications),Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper), Muondosha Mfanga (The Guardian).

Baadhi ya wanafunzi kutoka vyo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jana kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,ambao umewashirikisha Marais Wastaafu nane wa Afrika.
