MASWALI YALIYO ZUA UTATA KUHUSU UHALALI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo April 4, 2012

Kuna maswali kadhaa yanaulizwa katika mitandao mbalimbali ya mazungumzo na majadiliano kwenye intaneti.

Baadhi yanahitaji maelezo ya ufafanuzi na vifungu vya katiba kusimamia majibu hayo kikamilifu.

Yafuatayo ni mojawapo ya maswali hayo:

SWALI: Je, Wizara ya afya ni sehemu ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania? Ikiwa jibu siyo, je, chaguo la Dkt. Hussein Mwinyi
kuiongoza Wizara ya Afya kama Waziri si kukiuka sheria mama (Katiba)?

SWALI: Pamoja na kuwa Rais anayo mamlaka kwa mujibu wa sheria kuteua Wabunge 10, je ipo mamlaka katika Sheria Mama inayoruhusu kuteuliwa kuwa Waziri kabla kwanza ya kuapishwa kuwa Mbunge na kisha kuapishwa kuwa Waziri?

Yakiongezeka maswali mengine nitayaweka hapa.Kazi ni kwako Mtanzania Mzalendo kusimamia sheria zinazokuhusu katika maamuzi ya maisha yako katika nchi yako!
 
MWENYE MAJIBU ATUSAIDIE ....(TUPE MAONI YAKO)

Posted by Bigie on 11:43 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.