MAWAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAANZA KAZI RASMI

 
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif  Rashid  akisalimiana na kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Wizara huyo, kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Regina Kikuli
 Naibu Waziri Mh.Dkt Rashid akiwapungia mikono kuwasalimia watumishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na baadhi ya watumishi wa wizara yake mpya
  Mh. Dkt. Mwinyi akipokea vitendea kazi mara baada ya kuwasili rasmi kwenye ofisi yake mpya ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.Dkt Mwinyi amewataka wakurugenzi wa Idara,Taasisi, Wakala pamoja na wakuu wa Idara kuwa na ushirikiano ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo, aidha wawe makini na kasoro ndogondogo ili kuweza kuwa na majibu mazuri yatakayoweza kukidhi mahitaji ya wananchi
Naibu Waziri Mh.Dkt. Rashid akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti kwenye wizara hiyo.

Posted by Bigie on 5:56 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.