MPAKA SASA HII NDIO PESA ILIYOCHANGWA KWA AJILI YA KUMTIBU SAJUKI.

Baada ya watanzania kujitolea pesa za kwenda kumtibu India mwigizaji Sajuki, hatimae kiasi kilichochangwa na siku ya safari vyajulikana.

Wastara ambae ni Mke wa Sajuki,  amesema imefikia hatua ambayo ni nzuri na wanaweza kuondoka kwenda India japo pesa haijafikia yote.


Pesa iliyokua inatakiwa ni milioni 25 lakini iliyopatikana ni milioni 16 lakini tayari itawawezesha kusafiri kwenda India jumapili au jumatatu ijayo  kwa sababu pesa nyingine bado zinaendelea kukusanywa.

Wataondoka yeye, Sajuki pamoja na kaka wa Sajuki na watakaa India kwa wiki mbili lakini kama kutakua na mabadiliko yeyote atasema


Mwishoni mwa wiki iliyopita Wastara alithibitisha kuibiwa zaidi ya laki nane kwenye account ya pesa ya simu yake ya mkononi baada ya wajanja wa teknolojia kuzuia pesa zilizokua zinatumwa na watanzania kwenye simu yake, na walifanikiwa pia kuiba pesa zilizokuwemo kwenye account ya Wastara.

Posted by Bigie on 2:25 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.