NAMPONGEZA DEO FILIKUNJOMBE KWA USHUJAA WAKE

Ndugu Mpekuzi
 
Tunashuhudia ni jinsi gani wananchi wamechoshwa kufanywa wajinga na kuuendelea kushuhudia watu waliokabidhiwa dhamana ya kuliongoza taifa wanafanya madudu na kuachwa bila kukemewa wala kuulizwa eti kwa sabababu ni mawaziri au wakurugenzi.
 
Kitendo cha wanachi wa Ludewa kutoka vyama vyote bila kujali itikadi ya kidini wala siasa kumpokea kishujaa namna hii mbunge Deo Filikunjombe ni ishara tosha kuwa wananchi wanamjua nani anawawakilisha na nani amekwenda bungeni kupiga usingizi. 

Mie huwa najiuliza wakati mwengine HIVI KAZI YA WABUNGE NI NINI? na jibu langu kanipatia Deo. Tofauti na watu tuliowazoea kushikia mabango madudu kama vile Zitto, Slaa, Tundu Lissu, Mrema nk ,wote hawa ni wa upinzani lakini huyu Deo anatoka chama tawala CCM.
 
Ushujaa wa Deo umetokana na kushikia bango bila kuogopa mtu yoyote kwenye madudu ya EKELEGE na TBS ambao hadi leo tumeona waziri kang'oka lakini na tunajua kuwa EKELEGE naye anafuata huko. 

Mheshimiwa Deo akishirikiana na wabunge wa upinzani aliamua kuangalia zaidi maslahi ya wananchi kuliko kuangalia nafasi ya kupewa uwaziri kitu ambacho Watanzania wengi tumekizoea kuwa kama mbunge akiwa mnoko sana basi asahau kuja kuwa waziri.
 
Sio rahisi kumnyooshea kidole  waziri au mkurugenzi wa shirika la umma kwa sababu watu hawa ni wakubwa sana na wana mtandao mkubwa nikiwa namaanisha watu wanaowatii. Kwa kufanya hivyo, Mheshimiwa Deo aliamua ku risk hata maisha yake na kumuumbua EKELEGE live tena kwenye TV na baadae magazetini na bungeni bila woga.
 
Mie nampongeza sana Mheshimiwa Deo kwa ushujaa wake ambao umeonekana wazi hadharani.
Kama kuna mtu ambaye alitakiwa ashike wizara ya kukamata wale wanaofanya madudu basi nadhani Deo angepewa hiyo wizara au hata unaibu kwa sababu siku zote mwenye duka huwa anaweka mlinzi asiyeeogopa wezi na sio yule anayejikomba kwa wezi.
 
Leo hii Mheshimiwa Deo kapokelewa kama Yesu alivyoingia Nazareti kwa shangwe ni dalili tosha kuwa wananchi wamechoshwa na madudu kama yale yaliyotambaa kila kona ya TBS.
 
Ni mategemeao yetu kuwa mheshimiwa Deo kama alivyotuahidi hatalala kamwe mpaka wale wote waliofanya madudu wameshughulikiwa na kuwa atashirikiana na Waziri Kigoda kwa kumpa ushauri mzuri ili naye asije yakamkuta yaliyomkuta jamaa yangu Chami aliyedharau wabunge kitendo ambacho ni kudharau wananchi waliompigia kura.
 
Namalizia kwa kumuomba tena Waziri Kigoda kabla hajawa bize na kusahau, afanye fumigation TBS na Ofisini kwake ili kuua kunguni na papasi au viroboto vyovyote vilivyotambaa kwenye hizi ofisi.
 
WABUNGE WALITOA RIPOTI YA UKAGUZI WAO.
WABUNGE WALISHAURI EKELEGE AFUKUZWE KAZI
Lakini ushauri wa wabunge ulipuuzwa na Chami na ndio maana amevuliwa Uwaziri.
UKIDHARAU WABUNGE NI KUWADHARAU WALIOMCHAGUA!
Wako ,
Mjumbe.

Posted by Bigie on 1:50 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.