SPIKA: HOJA YA LEMA IMEKUFA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amesema kuwa kuondoka bungeni kwa aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kumeizika hoja yake ambayo ilikuwa ikingoja uamuzi wa kiti chake.

Lema ambaye alienguliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha hivi karibuni, alimtuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa alilidanganya Bunge kuhusu vurugu za Arusha Januari 5, mwaka jana, zilizosababisha vifo vya watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Licha ya Lema kutamba kuwa alikuwa tayari amepata vielelezo 23 vya kuthibitisha uongo wa Pinda bungeni kuhusu matukio ya vurugu za Arusha zilizofuatia uchaguzi wa meya wa jiji hilo, bado hoja yake ilikuwa imewekwa kiporo na Spika.

Akizungumza jana kwa njia ya simu na Tanzania Daima, Spika Makinda, alisema kimsingi baada ya mbunge huyo kuenguliwa ubunge na hoja yake hiyo imekufa.

Licha ya gazeti hili kutaka ufafanuzi zaidi wa ni kwa nini uamuzi wa kiti chake, unachukua muda mrefu kiasi ambacho kinaweza kuleta chuki baina ya pande zinazoshutumiana, Makinda alijibu kwa kifupi akisema, “Kasome kanuni zetu, Spika anaweza kutoa uamuzi wake palepale anapoombwa mwongozo au wakati atakaoona unafaa.”

Alipoulizwa ni lini pengine atazitolea ufafanuzi hoja hizo ambazo nyingine wahusika wake wameenguliwa ubunge, Spika alisema kuwa hilo la Lema liko wazi kuwa alipoondoka bungeni na hoja yake haipo tena.

“Kasome kanuni zetu uzielewe, unataka nitoe uamuzi wa kiti wapi? Nje ya vikao vya Bunge au? Nimekwambia kiti kitaamua muda unaofaa,” alisema Makinda na kukata simu yake.

Tanzania Daima ilimtafuta mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ambaye ni mmoja wa wabunge wanaosubiri uamuzi wa miongozo dhidi yao, kutaka kujua kama alishatakiwa kupeleka ushahidi wa tuhuma zake.

Kafulila alisema kuwa hadi sasa bado anasubiri uamuzi wa kiti kwani hajawahi kutakiwa kupeleka ushahidi wowote kuthibitisha tuhuma zake.

“Lakini mimi hapa ninachokiona ni udhaifu kwenye kanuni zetu maana zinasema Spika atatoa uamuzi wake pale pale au wakati wowote atakaoona unafaa ila hakuna ukomo wa muda maalumu. Utaona kuwa hoja yangu inakaribia mwaka sasa,” alisema Kafulila.

Juni 13, mwaka huu, wakati akichangia hotuba ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Kafulila, aliwatuhumu wabunge wenzake ambao walikuwa katika kamati ndogo ya LAAC 

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Posted by Bigie on 6:09 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.