MBUNGE WA BAHI APANDISHWA KIZIMBANI KWA MASHITAKA YA KUPOKEA RUSHWA


MBUNGE wa Jimbo la Bahi, Mkoani Dodoma, Omar Badwel, leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka mawili ya rushwa.

Akimsomea mashitaka yake, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Ben Lincoln, amesema mnamo Mei 30 mwaka huu, mshitakiwa akiwa Mbunge wa Jimbo la Bahi na Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, alimuomba rushwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Schola Jonathan, ili aweze kuwashawishi wajumbe wa kamati yake waweze kuipitisha taarifa ya fedha ya halmashauri hiyo.

Shitaka la pili alilosomewa ni kupokea rushwa, ambapo mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru amedai kuwa mnamo Juni 2 mwaka huu, mshitakiwa alinaswa kwenye Hotel ya Peacock jijini Dar, akipokea rushwa ya shilingi milioni moja kutoka kwa Schola. 

Mbunge huyo alikana mashitaka hayo mbele ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Faisar Kihamba, ambapo hakimu huyo aliiahirisha mpaka Juni18 mwaka huu, itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Posted by Bigie on 10:13 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.