TANGAZO MUHIMU KWA WAKAZI WA MOROGORO KUHUSIANA NA TATIZO LA MAJI LINALOWAKABILI HIVI SASA
habari za kitaifa 7:37 AM
Bomba kubwa linalotoa maji bwawa la Mindu kupeleka sehemu ya kutibia maji Mafiga lenye kipenyo cha inchi 24 (24") sawa na milimeta 600 (600mm) limepasuka sehemu mbili tofauti.
Bomba hili ndo linalosambaza maji mjini Morogoro zaidi ya asilimia 75.
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) inaendelea na juhudi za kulitengeneza bomba hilo kama inavyoonekana kwenye picha ili huduma ya maji ilejee haraka iwezekanavyo.
Shukrani za dhati kwa Rashid Bumarwa kwa kutupatia taarifa hii muhimu









