"SITAKI KUMWONA LORD EYEZ NYUMBANI KWANGU".......MAMA RAY C


MAMA mzazi wa staa wa Bongo Fleva mwenye skendo ya kubwia madawa ya kulevya, Rehema Chalamila  ‘Ray C’, Magret Mtweve ametoa tamko kali dhidi ya aliyekuwa mpenzi wa mwanae, Isaac Makuto ‘Lord Eyez’ kutotia mguu nyumbani kwake Kunduchi, Dar.


Mama Ray C alichimba mkwara huo wakati akizungumza na Mpekuzi wetu Jumatatu iliyopita alipoulizwa kama Ray C amerudi nyumbani kwake baada ya kutoweka kitambo.

“Amerudi jana jioni (Jumapili). Nilipomuuliza amesema alikuwa Kariakoo, lakini hataki kuwataja aliokuwa nao wala alichokuwa akikifanya.



“Nimekuwa nikizunguka kwenye makanisa mbalimbali kumuombea njia, naona ameanza kuleta matumaini lakini sitaki kabisa kumsikia mtu anayeitwa Lord Eyez, yeye na wenzake ndiyo waliomsababishia matatizo haya mwanangu,” alisema mama huyo.


Posted by Bigie on 12:09 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.