POLISI YAMWACHIA LORD EYEZ KWA DHAMANA MAALUM


.
Stori za uhakika nilizozipata muda mfupi uliopita ni kwamba mkali wa Hiphop kutoka A Town ambae alikua anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz, Isack Waziri (Lord Eyes) hivi sasa yuko nje kwa dhamana.
Ametoka nje kwa dhamana toka ijumaa ya novemba 2 2012.
Oktoba 23 2012 Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alikaririwaakisema “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia  kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”

Posted by Bigie on 4:48 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.