"TUNAOMBA JAMII ITUSAMEHE KUHUSU KASHFA ZA NGONO NA KUTUPOKEA UPYA".....SHAMSA FORD WA BONGO MOVIE


MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Shamsa Ford amewaomba wapenzi wa filamu wawapokee wasanii wa kundi la Bongo Movie unity baada ya kuundwa upya kufuatia kubadilisha uongozi uliopita kushindwa kulinda nidhamu na maadili ya Mtanzania na kukumbwa na kashifa za ngono na kuteka vyombo vya habari kwa habari mbaya tu.

“Ni kweli kuna wenzetu ambao wametuchafua kweli kutokana na mambo yao ya ajabu, lakini sisi tunaojielewa tunaomba jamii itupokee kama wasanii wao tunaowategemea wao kama mashabiki wetu na tunawahitaji sisi ni sawa na mtoto akichafuka mkono hauwezi kukatwa, tunahitaji kusamehewa kutokana na watu wachache wasio na maadili mema’”anasema Shamsa.

Msanii huyo ambaye amekiri kwa kusema kuwa kundi hilo kwa sasa limechafuka katika jamii ni kutokana na tabia mbaya za wasanii wachache ambao inawezekana nyuma ya pazia kuna biashara nyingine wanayotegemea ndio maana wanafanya upuuzi unaowatukanisha wanawake waliopo katika tasnia ya filamu na jamii kuwapuuzia kama ni watu wasiojitambua.

Posted by Bigie on 7:27 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.