BREAKING NEWS: MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE ( KASHI) AFARIKI DUNIA LEO MCHANA
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, kashi 7:59 AMMuigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) amefariki dunia leo mchana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, Tamu Chungu akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde,Samson na wengine.
Baada ya kupata habari hii, mwandishi wetu aliongea na muigizaji mwenzake Monalisa ambae amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Monalisa amesema alipata taarifa jana kwamba Kashi amelazwa hospitali akiwa amezidiwa kiasi cha kushindwa kuongea na hivyo kushindwa kujua nini kilikuwa kinamsumbua.
Naye Hemedy PHD ametweet: REST IN PEACE MUIGIZAJI MWENZETU JAJI KHAMIS KASHI….MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI…MOVIE YA MWISHO TULICHEZA WOTE ILIKUA MATILDA!!Sad newz
BAADA YA KUJIUZA KWA MIAKA KADHAA, AUNT LULU WA BONGO AAMUA KUBADIILI UPEPO WA MAISHA
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, PICHA ZA UCHI 3:41 AMSiku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya.
Akiongea na mwandishi wa habari hii, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.
“Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa.
Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani.
Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, Dar ambapo ndipo anashinda kwa sasa na kwa mujibu wake ameachana kabisa na kujiachia kwenye sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.
MZEE CHILO AWACHANA LAIVU WASANII WANAOVAA NUSU UCHI
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 12:43 AMSTAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Uloto ‘Mzee Chilo’ amewachana wasanii wa filamu wanaovaa nusu uchi huku akieleza kuwa, kufanya hivyo ni kuiabisha tasnia ya fimlamu Bongo.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Mzee Chilo alisema amekuwa kwenye tasnia hiyo kwa muda mrefu sana na kuwashudia wasanii kama vile Suzan Lewis ‘Natasha’ na mama Mjata wakiigiza filamu zao kiheshima lakini siku hizi anashangazwa na uvaaji unaokiuka maadili, si kwenye filamu tu bali hata kwenye maisha yao ya kila siku.
“Mbona kuna hawa wakongwe ambao wanaigiza vizuri na kufikisha ujumbe bila kuvaa nusu uchi? Kwa kweli hali sasa hivi ni mbaya na wasanii hasa wa kike wanatakiwa kujirekebisha wanapokuwa wanaigiza na hata kwenye maisha yao ya kawaida,” alisema Mzee Chilo.
ZIFF YAKERWA NA USHIRIKI MDOGO WA FILAMU ZA TANZANIA
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 3:29 AMWaandaaji wa tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar, ZIFF wamedai kusikitishwa na muitikio hafifu wa waigizaji wa filamu Tanzania katika kuwasilisha filamu zao.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ZIFF imedai iliitisha upokeaji wa filamu kwaajili ya tamasha la 16 la nchi za Jahazi Septemba 2012 na kuweka mwisho wa kupokea kuwa ni tarehe 31 Machi, 2013 lakini wamepokea filamu chache kutoka Tanzania ukilinganisha na za nje. Jumla ya filamu 200 zimeshawasilishwa mpaka sasa lakini filamu za Tanzania ni tano pekee.

“Filamu za Tanzania ambazo tumepokea mpaka sasa hazi zidi 5 ukijumla na zile zinazoingia katika uchaguzi wa jumla (General Selection) na zile kwajili ya Swahili Movie/Bongo Movie competition,” imesema taarifa hiyo.
“Tukumbuke filamu hizi ndio zitatoa Filamu Bora ya Kitanzania na pia kugombea Filamu Bora ya Afrika Mashariki na maeneo mengine Tumekuwa wavivu wa kusoma websites, blogs na hata magazeti kwa kutegemea kupata taarifa za mdomo au taarifa kwa mtu mmoja mmoja ili kujua nini kinaendelea, jambo ambalo si sahihi, tujifunze kupitia vyombo vya habari ili tupate habari kwa wakati muafaka,” imeendelea kusema taarifa hiyo iliyoandikwa meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi.
“Hivyo basi natoa nafasi mpaka tarehe 15 Aprili, 2013 filamu zote za Kitanzania ziwe zimetumwa ZIFF au kupatiwa Ndugu Ibrahim Mitawi (Outreach Officer) – Dar es Salaam (0713-300997) au Mohamed (Film Coordinator) – Zanzibar (0718115468).”
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ZIFF imedai iliitisha upokeaji wa filamu kwaajili ya tamasha la 16 la nchi za Jahazi Septemba 2012 na kuweka mwisho wa kupokea kuwa ni tarehe 31 Machi, 2013 lakini wamepokea filamu chache kutoka Tanzania ukilinganisha na za nje. Jumla ya filamu 200 zimeshawasilishwa mpaka sasa lakini filamu za Tanzania ni tano pekee.

“Filamu za Tanzania ambazo tumepokea mpaka sasa hazi zidi 5 ukijumla na zile zinazoingia katika uchaguzi wa jumla (General Selection) na zile kwajili ya Swahili Movie/Bongo Movie competition,” imesema taarifa hiyo.
“Tukumbuke filamu hizi ndio zitatoa Filamu Bora ya Kitanzania na pia kugombea Filamu Bora ya Afrika Mashariki na maeneo mengine Tumekuwa wavivu wa kusoma websites, blogs na hata magazeti kwa kutegemea kupata taarifa za mdomo au taarifa kwa mtu mmoja mmoja ili kujua nini kinaendelea, jambo ambalo si sahihi, tujifunze kupitia vyombo vya habari ili tupate habari kwa wakati muafaka,” imeendelea kusema taarifa hiyo iliyoandikwa meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi.
“Hivyo basi natoa nafasi mpaka tarehe 15 Aprili, 2013 filamu zote za Kitanzania ziwe zimetumwa ZIFF au kupatiwa Ndugu Ibrahim Mitawi (Outreach Officer) – Dar es Salaam (0713-300997) au Mohamed (Film Coordinator) – Zanzibar (0718115468).”
KWA NINI MAMISS WA TANZANIA HAWAOLEWI NA BADALA YAKE HUTUMIWA NA KUACHWA
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 10:45 AMWAKATI mashindano ya u-miss yanaanzishwa Bongo, wazazi wengi walikuwa wazito kuwaruhusu watoto wao kushiriki wakiamini kwamba ni uhuni. Kadiri miaka ilivyozidi kusonga mbele, taratibu walianza kuelewa kuwa siyo uhuni na wakawaruhusu watoto wao kwa kuyaona yana tija.
Matunda ya warembo yalionekana, lakini kumekuwa na dosari kwao, licha ya mafanikio makubwa wanayoyapata, asilimia kubwa hawaolewi. Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini hawaoleki, why?
Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema, sababu inayosababisha warembo hawa wasiolewe au hata wakiolewa wasidumu kwenye ndoa ni jinsi wenyewe walivyojijenga akilini kuwa ni watu maarufu, wazuri hivyo wamekuwa wakichagua wanaume na kuishia kutumiwa, wakija kushtuka umri unakuwa umewatupa.
MSANII WA BONGO MOVIE AKAMATWA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 1:45 AM
STAA wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni aliswekwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji mwenzake .
Akizungumza na waandishi wetu, Lungi aliyesota mahabusu kwa siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane aligongewa mlango nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa kwa ujambazi.
Hata hivyo, Lungi alisema kuwa baada ya kuwauliza askari ni wapi dada huyo amevunjiwa au kitu gani alichoibiwa, askari walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana.
STAA WA FILAM BONGO AKUMBWA NA BALAA BAADA YA KUJIKUTA AKILEA "MTOTO MCHAWI"
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 4:25 AMKELVIN....
STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Khalfan ‘Kelvin’ na mkewe mwigizaji, Elizabeth Chijumba ‘Nikita’ wamesema mmoja wa watoto pacha waliowaasili (adopt) mwenye umri wa miaka sita, ameonesha matendo ya kichawi...
Akizungumza na mwandishi wetu, Kelvin alisema waliwachukua watoto hao mapacha kwa bibi yao Mtwara mwaka 2009 kwa lengo la kuwalea kutokana na mazingira magumu waliyokuwa nayo lakini walipofika Dar, mmoja alianza kuonesha vitendo tofauti vya kichawi.
“Wakati tukiendelea kuishi nao, tulimuona mmoja ana vitukovituko mara kwa mara na tuligundua kuwa mke wangu alikuwa akiumwaumwa kila alipomgombeza mtoto huyo.
“Kuna siku niliamka usiku kwenda kwenye chumba walichokuwa wakilala watoto hao, nikamkuta akiwa uchi akirukaruka kitandani na nilipomshtua alijilaza kitandani na asubuhi tulipomuuliza, alisema muda ule bibi yake alikuwa akimrudisha kutoka kuroga Tanga."
Kwa upande wake, Nikita alipomdadisi mtoto huyo kuhusu vitendo hivyo vya kichawi, alimwambia kuwa bibi yake anataka kumuua kwa sababu wanamzuia asirudi kijijini kwao Mtwara akaendelee kufanya kazi za kichawi.
“Kwa kweli nampenda sana lakini sina budi kumrudisha nyumbani kwao, roho inaniuma kwa sababu nilimzoea,” alisema Nikita.
Mwandishi wetu alipomuuliza mtoto huyo kuhusiana na sakata hilo, alikiri kuwa ni kweli bibi yake ni mchawi na huwa anamchukua kwenda sehemu mbalimbali kuroga kwa kutumia usafiri wa ungo na ndiye anayemroga Nikita.
TYSON AELEZEA SABABU ZINAZOICHAFUA TASNIA YA FILAMU
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 9:05 AM
Kutokana na kashfa ya rushwa ya ngono kuikumba tasnia ya filamu Tanzania mtayarishaji wa filamu nchini Geoge Tyson aelezea chanzo cha rushwa hiyo ni kutokana na ukosefu wa elimu kwa baadhi ya waandaaji wa filamu nchini
Akizungumza jijini Dar es Salaam Tyson alisema kuwa rushwa inachangiwa na waandaaji wa filamu kukosa maadili ya kazi na hali ambayo imesababishwa na kukosa elimu ya uaandaaji wa kazi hiyo na matokeo yake kuchukua watu wasio na sifa na kipaji cha uigizaji
Tyson aliweka wazi kuwa wengi wa waandaaji hao wamepata uzoefu wa kile wanachokifanya kupitia kazi walizokuwa wakifanya hali inayochangia unyanyasaji kwa watu wengine wenye sifa ya kuwa waigizaji na ndio maana katika tasnia hiyo imejaa wababaishaji na siyo wenye vipaji
"Ukiwa msichana mrembo na mwepesi kutongozeka ni rahisi kupata nafasi ya kuigiza ila ukiwa mgumu na wa kawaida hata kama unakipaji siyo rahisi kupata nafasi ya kuigiza kitu ambacho si kizuri kwa ajili ya kukuza fani ya uigizaji" alisema Tyson
Pamoja na hayo aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya waandaaji wanatumia kambi kama njia ya kurahisisha kukutana kingono na baadhi ya washiriki wa filamu, wakati hapo mwanzo hakukuwa na maswala ya kambi na hakuna umuhimu wa kuwa na kambi
Tyson alielezea jinsi kambi zilivyokuwa hazina umuhimu kwenye tasnia ya filamu na kutoa mfano kuwa watu wenye umuhimu wa kuwa na kambi ni wacheza mpira
PR0-24 blog
MAMA STEVEN KANUMBA AJA NA FILAMU YA "WITHOUT DADDY."
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, kanumba 11:52 PMMAMA Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba’ Frola Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye baada ya kuigiza katika filamu ya Without Daddy akishirikiana na watoto waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na Jamila, katika filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.
.
Ben Blanco akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
Mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika Filamu ya Without Daddy.
Mama Kanumba mwigizaji.
Filamu ya Without Daddy imeshirikisha wasanii nyota wengi kama vile Abdalah Mkumbilah ‘Muhogo mchungu’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ Cathy Rupia, Mayasa Mrisho, ‘Maya’, Othuman Njaidi ‘Patrick’ Wastara Juma ‘Stara’ Abdul Ahmed ‘Ben Blanco’ na wasanii mahiri wengineo.
.
Ben Blanco akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.Akiongea na FC mkurugenzi wa kampuni ya Big Daddy Production Irene Kaungwa amesema kuwa filamu ya Without Daddy ni kazi mwendelezo wa kazi ya marehemu Kanumba iliyotoka siku za nyuma ya Big Daddy na ni kazi ambayo imetentengezwa kwa ubora wa kimataifa ikiwa sambamba na kumtambulisha mama Kanumba katika tasnia ya filamu Swahiliwood.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
Mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika Filamu ya Without Daddy.
Mama Kanumba mwigizaji.TIMBULO WA "LEO WA KESHO" AINGIA BONGO MOVIE
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, rose ndauka 9:41 AM| Moja ya picha ya Timbulo na Rose Ndauka wakiwa location |
| -------------------------- |
Msanii wa bongo fleva Ally Timbulo maarufu kama Timbulo ivi sasa yuko katika michakato ya kufanya movi ambayo inaitwa "Ulimwengu wa faida" lakini pia katika movi hiyo wako mastaa wengine kibao kama Mzee Chiro, Hemed PHD huku Rose Ndauka pamoja na timbulo ndo watakua wahusika wakuu katika movi hiyo.
Msanii huyo ameamua kuingia katika bongo movi baada ya comenti nyingi sana kutoka kwa mashabiki wake kuwa anauwezo wa kufanya filamu kutokana na vipande ambavyo huwa anaigiza katika video zake za muziki.
Harakati za bongo.
Harakati za bongo.
HEMED PHD NDANI YA "TOP 20 COUNTDOWN" YA CHOICE FM LEO JIONI
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, HEMEDY 4:45 AMKama wewe ni shabiki wa Hemed Phd basi leo hupaswi kukosa kumsikiliza akitangaza kipindi cha The Countdown cha nyimbo 20 kupitia Choice Fm ya Dar es Salaam.
Kipindi hicho huruka kuanzia saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni.Choice Fm husikika Dar es Salaam pekee kupitia 102.5 FM na kwa njia ya internet.
HII NDO TRAILER YA MOVIE MPYA YA DR. CHEN.."HUKUMU YANGU"
Posted by Bigie BONGO MOVIE, DR CHEN, habari za kitaifa 6:07 AMMsanii wa Bongo movie maarufu kama Dr Cheni baada ya mwaka jana kufanya vizuri katika industries ya filamu,sasa mwaka huu amejipanga upya.
Dr Cheni sasa yuko katika hatua ya kuachia movie yake mpya inayokwenda kwa jina la “Hukumu Yangu”.Wasani mahiri walioshiriki katika movie ni Mzee Onyango na wasanii wengineo.
WASANII WA FILAMU BONGO KUPELEKWA NIGERIA
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa 11:17 PMMkurugenzi wa Mad Mad Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano hupo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
Wasanii wa Bongo Movies wana nafasi ya kuongeza wigo wa kazi zao katika soko la kimataifa baada ya kampuni ya Mad Mad Entertainment ya nchini Uingereza kuanzisha mchakato wa kupeleka wasanii wa tasnia hiyo nje ya nchini.Lengo la mpango huo ni katika jitihada za kuikuza tasnia hiyo nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Yasmin Razak kwa muda mrefu aliokaa nchini Uingereza hajaona kama kuna maendeleo kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Razak alisema ndio maana ameamua kuanzisha mradi huo ili kuikuza sanaa hiyo.
“Katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini,” alisema.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo.”
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Yasmin Razak kwa muda mrefu aliokaa nchini Uingereza hajaona kama kuna maendeleo kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Razak alisema ndio maana ameamua kuanzisha mradi huo ili kuikuza sanaa hiyo.
“Katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini,” alisema.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo.”
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
"NIMECHOKA KUSEMWA...ANAYETAKA KUJUA JINSIA YANGU AVUE TWENDE KITANDANI"...ZAHARA CHAMBO WA BONGO MOVIE
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, ZAHARA CHAMBO 9:54 AMMUONEKANO wa mwigizaji wa filamu za Kibongo anayefamika kwa jina la Zahara Chambo, umezua utata baada ya watu kudai kuwa ana jinsia ya kiume huku wengine wakidai ni mwanamke.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwigizaji huyo amewahi kuwa na uhusiano na mastaa kibao wa kike Bongo, lakini wote wamekuwa wazito kutoa majibu sahihi juu ya jinsia ya msanii huyo.
“Mastaa wengi tu wa kike wamekiri kuwa ‘wameshatoka’ naye lakini hawafunguki juu ya jinsia yake na namna ambavyo amewaridhisha kimapenzi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Wapo wengine wanadai eti ni mwanamke na huwa anawafanyia wenzake mchezo mchafu.”
Baada ya kuyasikia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Zahara kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa na uhusiano na wanawake mbalimbali huku akidai huwa wanamfuata wenyewe.
“Huwa wanajilengesha kwangu kwa makusudi ili wajue kama nina jinsia ya kiume au ya kike lakini ukweli naujua mwenyewe, kama mtu anataka twende kitandani,” alisema Zahara.
Aidha aliongeza kuwa, kuna wakati wanawake wanaogopa kufanya naye kazi kwa kumhofia kuwa anaweza kufanya nao mapenzi kitu ambacho anasema hakina ukweli kwani na yeye ana mpenzi wake ambaye anampenda sana.
“Kwa hivi sasa mimi nina mtu wangu mmoja (hakutaja jinsia yake) ambaye ananipenda kuliko chochote, nashangaa kuona watu wengine wanaogopa kufanya kazi na mimi bila sababu za msingi,” alisema Zahara.
"RAY HAIJUI HATA NGUO YANGU YA NDANI....NAOMBA NIWEKE WAZI KUWA SI MPENZI WANGU"...SAJENT
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, ray 9:12 AMBAADA ya ishu kuvuja kuwa msanii wa filamu Husna Idd ‘Sajenti’, ana mahusiano ya kimapenzi na ’Ray’, amezikana habari hizo huku akisisitiza kuwa msanii huyo anamchukulia kama kaka yake na suala la kutoka naye kimapenzi halina ukweli wowote.
Tukio la Sajenti kutoka na Ray lilianza kuskika pindi kundi la bongo movie lilipoenda mkoani Mwanza kucheza mchezo wa kirafiki na wasanii wa mkoani humo.
Mtandao huo ulitaka kujua Sajenti anazungumziaje habari hizo, ambapo alidai kuwa hajawahi kutoka na ’Ray’ kimapenzi na anayesambaza ishu hizo ana nia ya kumchafua ingawa alishindwa kueleza anachafuliwa kwa namna gani.
Alisema kuwa kama zingekuwa na ukweli taarifa hizo angeweka wazi lakini haoni sababu ya kukubali wakati kitu hajawahi kukifanya na wala hana wazo wa kutoka na msanii huyo kwani mpenzi wake anamtosha.
“Sijawahi kutoka kimapenzi na Ray na hajui hata nguo yangu ya ndani na kama una ukweli kama unajua natoka naye kwanini umepiga simu na kuniuliza,??.. nasema sijawahi kutoka naye,” alidai.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa kama mwanaume aliwahi kutoka naye hawezi kuficha lakini juu ya Ray atakanusha siku zote.
Tukio la Sajenti kutoka na Ray lilianza kuskika pindi kundi la bongo movie lilipoenda mkoani Mwanza kucheza mchezo wa kirafiki na wasanii wa mkoani humo.
Mtandao huo ulitaka kujua Sajenti anazungumziaje habari hizo, ambapo alidai kuwa hajawahi kutoka na ’Ray’ kimapenzi na anayesambaza ishu hizo ana nia ya kumchafua ingawa alishindwa kueleza anachafuliwa kwa namna gani.
Alisema kuwa kama zingekuwa na ukweli taarifa hizo angeweka wazi lakini haoni sababu ya kukubali wakati kitu hajawahi kukifanya na wala hana wazo wa kutoka na msanii huyo kwani mpenzi wake anamtosha.
“Sijawahi kutoka kimapenzi na Ray na hajui hata nguo yangu ya ndani na kama una ukweli kama unajua natoka naye kwanini umepiga simu na kuniuliza,??.. nasema sijawahi kutoka naye,” alidai.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa kama mwanaume aliwahi kutoka naye hawezi kuficha lakini juu ya Ray atakanusha siku zote.
WEMA SEPETU AJIKUTA AKIWAKUMBATIA WAZEE AKIKWEPA KUGUSWA NA "PANZI"
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, wema sepetu 9:52 AMKATIKA hali isiyo ya kawaida ya kutozoea maisha ya kijijini, msanii asiyeishiwa matukio, Wema Sepetu, hivi karibuni alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuwakumbutia wazee wa kijijini akikwepa panzi pindi walipokuwa katika ziara ya uzinduzi wa mpango wa Kilimo Kwanza kwa vijana eneo la Kwandelo, Kondoa.
Wakati wakiwa katika harakati za kuhamasisha kilimo kwanza , panzi alianza kuruka ruka eneo hilo ambalo ni sehemu ya shamba hali iliyomchanganya msanii huyo na kuanza kukimbia hovyo huku akijifunika usoni na mkoba wake akikimbilia sehemu waliyokuwa wamesimama wazee.
Hata hivyo baada ya kurejea Dar mwandishi wetua alizungumza na mrembo huyo ambaye alisema kuwa hakuwai kumuona mdudu huyo hivyo hali hiyo ilimpa wasiwasi mkubwa kwa kuhisi anaweza kudhuliwa afya yake
JACK WA CHUZ AIKANA MIMBA YAKE.....
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, JACK WA CHUZ 1:21 AMMSANII wa sinema za Kibongo Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ amekanusha habari zinazosambaa mitaani kwamba ana ujauzito.
Picha hizo ziliingizwa katika mtandao huo na msanii mwenzake Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye baadaye alithibitisha kwamba Jack ni mjamzito....
“Kama unavyoniona niko fiti na sina mimba, zile picha tumepiga kwa ajili ya filamu na hakuna kitu kama hicho, wala sitarajii kuwa na mimba kwa siku za hivi karibuni,” alifafanua Jack .
"NAWACHUKIA SANA WASANII WA KIUME WANAOJICHUBUA"...MZEE MAGALI
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, MZEE MAGALI 1:14 AMMSANII nguli wa filamu za Kibongo, Charles Magali ‘mzee Magali’ amesema kuwa anachukizwa na tabia ya baadhi ya wasanii wa kiume wa filamu wanaojichubua na kuweka dawa nywele zao.
Akizungumza na na mwandishi wa habari hii, mzee Magali alisema kwa muda mrefu amekuwa akilikemea jambo hilo bila ya mafanikio.
“Wasanii ni kioo cha jamii, hebu waseme wanapata faida gani wanapofanya hivyo zaidi ya kuhisiwa tofauti na jamii? Mbona wanaweza kuwa wasanii wazuri bila ya kujichubua na kuweka dawa nywele zao?” alihoji.
HUU NDO UHASAMA NA CHUKI BINAFSI ZA WASANII WETU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2012
Posted by Bigie BONGO FLEVA, BONGO MOVIE, habari za kitaifa 4:20 AMTID vs Ali Kiba
Beef hii ilianza baada ya Ali Kiba na familia yake kumshutumu TID kuwa alikuwa amepanga njama za kumuua Ali Kiba. Tuhuma hizo zilipelekea TID kupelekwa polisi lakini alitoka baada ya kesi hiyo kuonekana haina ushahidi wa kutosha.
Mpaka sasa TID bado ana hasira na Ali Kiba na hivi karibuni kupitia Facebook alimuita ‘homo’ kutokana na kitendo chake cha kumtupia shutuma hizo. “Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him while am only thinkin about this Girl…No Homo,let’s make Hits,” aliandika TID.
AY vs Hermy B

Uhusiano kati ya Hermy B na AY waliokuwa maswahiba wa muda mrefu uliingia dosari baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kuelewana katika bei mpya ya kurekodia wimbo katika studio za B’Hits.
Hermy B aliwataka AY na MwanaFA kulipia kiwango kikubwa zaidi kwa single wanazorekodi kwakuwa wao ni wasanii wakubwa kitu ambacho hawakukikubali na kuamua kuvunja uhusiano na B’Hits. Baadaye Hermy B alikuja kuandika barua mbili tofauti kuelezea jambo hilo na jinsi uhusiano wao ulivyovunjika.
AY alidai angekuja kuandika maelezo kwa upande wake lakini hata hivyo hakuandika. Miongoni mwa aliyoandika Hermy kwenye barua ya kwanza ni:
Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa kawaida anaehangaika kutoka.
Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi, ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja niliomba nilipwe millioni 2.
Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na niliona biashara hii itavunja urafiki wetu.
Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya. Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo bado hazijamixiwa, ila ampatie producer mwingine amfanyie hiyo kazi.
Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi.
Lord Eyez vs Ommy Dimpoz

Beef hii ilianza baada ya Ommy Dimpoz kupost picha za Lord Eyez kwenye mtandao wa Twitter akiwa amekamatwa kwa kile alichodai kumuibia vifaa vya gari yake. Picha hizo zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na websites/blogs.
Baadhi ya watu walimlaumu Ommy kwa kitendo hicho cha kumwanika mwanamuziki mwenzie. Baada ya kukamatwa na polisi na baadaye kutoka nje kwa dhamana wakati kesi hiyo ikiendelea, Lord Eyez alirekodi wimbo Bongo Records ambamo anasikika akimtaja Ommy Dimpoz.

Beef ya chini chini kati ya Weusi na Nikki Mbishi ilianza kitambo na ilitokana zaidi na mistari ya Nikki Mbishi aliyoindika kumdiss Bonta wa Weusi kama msanii anayebahatisha na sio conscious rapper kama anavyojiita.
Hivi karibuni Nikki wa Pili alisikika kwenye mstari wake akitupa diss ya kiaina kwa Nikki Mbishi na washkaji zake kwa kusema yeye haandika punchline bali anaandika maisha.
Irene Uwoya vs Flora Mvungi

Beef ya divas hawa Bongo Movies ilitokana na uhusiano wao na H Baba. Baada ya H Baba kuachana na Irene alianzisha uhusiano na Flora waliye naye hadi sasa.
Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari Irene alisikika akimponda H Baba kuwa ni mwanaume asiyejua mapenzi. Kauli hiyo ilimkera Flora ambaye naye aliamua kuongea yake na hivyo kuanzisha beef na Irene.
Afande Sele vs 20 Percent
Maswahiba haba walijikuta wakizunguana na kutupiana maneno redioni kutokana na Afande kukerwa na kitendo cha 20 Percent kugombana na waandaji wa tuzo Zanzibar waliokuwa wamewaalika wote.
Cyril vs Ommy Dimpoz

Ilikuwa ni beef iliyodumu kwa muda mfupi baada ya uzinduzi wa documentary ya Cyril ‘From Day One’ uliokuwa umepangwa kufanyika Club Billcanas kutaka kuzuiwa na baraza la sanaa Tanzania kwa madai kuwa ni raia wa Kenya. Jambo hilo Cyril aliliona kama hujuma iliyokuwa imepangwa na Ommy aliyekuwa na show siku hiyo hiyo Maisha Club.
Chidi Benz vs Ney wa Mitego

Pamoja na kuanzisha beef kali na waigizaji wa Bongo Movies kutokana na wimbo wake Nasema Nao, Ney wa Mitego alimdiss pia King Kong Chidi Benz kwa kuamua kujitoboa pua na kuweka heleni. “Au mwenzetu shoga” alisema Ney kwenye ngoma hiyo.
Kwa upande wake Chidi Benz baada ya kuhojiwa ili aseme alivyouchukulia mstari huo na kusema hamfahamu Ney wa Mitego.
Diamond vs H Baba

Beef ya Diamond na H Baba ilitokana na wimbo ‘Nataka Kulewa’ wa Diamond. H Baba alidai kuwa Platnumz alimuibia idea hiyo wakati walipokuwa wakirekodi wimbo wenye jina kama hilo katika studio za G Records ambapo alikuwa amepanga kumshirikisha Q Chief. H Baba alionesha vielelezo vyote kuthibitisha kauli yake licha ya baadhi ya watu kudai anataka umaarufu.
Q Chief vs Adam Juma
Hii ni beef ya hivi karibuni tu ambapo Q Chief anamshutumu Adam Juma kwa kutoitoa video yake aliyomfanyia. Q analaumu kuwa Adam amemharibia mipango yake na huku akimrudisha nyuma kimaendeleo.
SOURCE
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...


















