UGONJWA WA MOYO WAMTESA SNURA
habari za kitaifa, snura 11:48 PM
HALI ya msanii kiwango wa filamu za Kibongo, Snura Mushi ‘Snura’ siyo nzuri kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa Moyo.
Akizungumza na paparazi wetu aliyemtembelea msanii huyo hivi karibuni nyumbani kwake, Mwananyamala, Dar es Salaam baada ya kupata taarifa ya kuumwa kwake, msanii huyo alisema anaumwa sana.
Aliongeza kwamba, tatizo hilo lilimuanza alipokwenda Muheza, Tanga kuhudhuria msiba wa Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’.
“Yaani sina hamu ya kula, kutapika ndiyo huku, sijui ni hizi dawa za malaria nilizomeza ndiyo zinasababisha hali hii, naumwa sana jamani...niombeeni kwa Mungu nipone,” alisema Snura.






