BAADA YA "NATAKA KULEWA"....DIAMOND SASA AANZA KUPIKA NGOMA MPYA NDANI YA AM RECORDS



Umepita muda mrefu tangu kuzuka kwa ile scandal kubwa iliyomwandama Diamond na producer wake Manecky ya kudaiwa kuiga idea ya nyimbo za H Baba na Pasha. 

Licha ya kuamua kufanya video ya wimbo huo ulioleta maneno mengi, Nataka Kulewa, Diamond aliamua kuupotezea na kuachia ngoma nyingine iliyotengenezwa na Marco Chali, ‘Kesho’ ambayo video yake iliyofanyika nchini Kenya chini ya Ogopa Djs ikiwa miongoni mwa video kali kabisa zilizotoka hivi karibuni.


Na sasa Diamond na Manecky wamekutana tena kufanya kile wakifanyacho kwa ubora. Kupitia website yake, Diamond ameweka picha akiwa AM Records na Manecky na kuandika:
manecky 2

"Leo tangia nimeamka nilikuwa na Mzuka wa kufanya ngoma…Nikaona sio kesi ngoja nimvutie waya Maneck…

Eeeeh! nasasa hali iko hivi hapa Am Rec. Ni moja ya wimbo wa tofauti sanaaaa.."

Posted by Bigie on 10:50 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.