DIAMOND ALAZIMIKA KUIPIGA CHINI TOUR YAKE YA UINGERTEZA BAADA YA PROMOTA WAKE KUZINGUA KULIPA....


Diamond amelazimika kuipiga chini tour yake ya barani Ulaya iliyokuanza ianze kwa show moja  March 9 jijini Stuttgart nchini Ujerumani. 



Taarifa hiyo imetolewa na Diamond kupitia website yake.

“Kutokana na kampuni ya United Events Ltd Tilburg-The Netherlands kwa upande mwingine kama promoter kushindwa kutimiza baadhi ya mahitaji ikiwemo kushindwa kulipa pesa ya show ambayo ilitakiwa ifanyike Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/Germany 09/03/2013 na zingine kama East African Night ambayo ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/Holland tarehe 15/03/2013 na kadhalika, mimi na team yangu nzima ya wasafi hatutoweza kuhudhuria kwenye events hizo,” amesema diamond kwenye maelezo yake.

“Nilikuwa nikipata Maswali mengi sana toka kwa mashabiki zangu mbalimbali wakiniuliza kuhusiana na ujio wangu wa nchi hizo za EUROPE lakini siku zote nilikua kimya sikuweza kujibu wala kuzungumza chochote na Wadau wangu kutokana na kutokuwa na uhakika wa tour hiyo.”

Posted by Bigie on 7:14 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.