HUDUMA YA "AIRTEL MONEY" YAZINDULIWA MJINI DODOMA KWA SHANGWE KUBWA USIKU WA KUAMKIA LEO
JAMII 7:15 PM
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Halisi kutoka TMK,likiongozwa na Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo,kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,uliofanyika jana jioni kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wati kibao.

Mmoja wa sanii mahiri wa miondoko ya hip hop hapa bongo,Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akiwapagawisha baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika jana jioni kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wati kibao.

Anajiita Simba Dume ndani ya msitu mnene,ni mmoja ya Wasanii wakongwe wa hip hop hapa nchini,ndani ya miondoko ya muziki wa kizazi kipya,Mfalme wa rhymes Afande Sele pichani kati akiwa amezungukwa na washabiki wake,huku akiwaimbia wimbo wake wa Karata Dume, shangwe na miluzi ikiwa imetawala uwanjani hapo jioni ya leo,wakati kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Money kwa wakazi wa mji wa Dodoma jana jioni

Wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money kutoka kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel wakishangilia

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Q-Chilla a.k.a Savimbi akiwaimbisha washabiki wake jana jioni kwenye uwanja wa Jamhuri wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money.

Mmoja wa wasanii wa miondoko laini laini hivi,aitwaye Mr Blue a.k.a Kabaisa akitumbuiza jukwaani jana jioni kwa wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la uzinduzi wa Airtel Money.

Namna shangwe za Aitel Money zilivyokuwa zikilindima usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
