WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MUHAS WAENDESHA MGOMO SIKU YA MAHAFALI ILIYOFANYIKA JANA MBELE YA RAIS MSTAAFU,NDG ALLY HASSAN MWINYI


Wakuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS) wakiingia kwa maandamano kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo hicho kabla ya kuzuka kwa vurugu.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS) wakimsikiliza mwenzao kabla ya kusambalatishwa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi (FFU).
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mh. Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiongozana na baadhi ya wakuu wa Chuo hicho mara baada ya kuzuka kwa vurugu za wanafunzi wa chuo hicho waliokiwa wakitaka kurudishwa kwa Serikali ya Wanafunzi ambayo ilivunjwa hapo awali.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akiwa ametiwa mbaroni

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS), leo wamesababisha shughuli za Mahafali ya Tano ya Chuo hicho kusimama kwa muda baada ya kuzuka kwa fujo kubwa zilizopelekea Askari wa Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kishindo ili kuwatawanya.

Wanafunzi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kurudisha serikali ya wanafunzi (MUHASSO).

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Deogratias Ntukumazina alitoa ahadi kwa wanafunzi hao ya kuirudisha Serikali ya Wanafunzi pindi watakapofuta kesi waliyofungua Mahakama Kuu kauli ambayo ilipingwa vikali na wanafunzi hao na kutishia kuvuruga shughuli za mahafali zilizokuwa zimesimama kwa muda kutokana na wanafunzi hao kufanya mkutano wao uongozi wa Chuo mbele ya Jukwaa ambalo sherehe za kuwatunuku wahitimu zingefanyika kutokana na kugoma kuondoka mahali hapo hata baada ya uongozi wa Chuo kuwataka kufanya hivyo jambo ambalo lilisababisha Jeshi la Polisi kuongeza nguvu ili kuwatawanya.

Hali ilivyokuwa mbaya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alitoa amri kwa Polisi waliokuwa wakilinda Usalama kutumia nguvu jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wazazi waliofika katika mahafali hayo kukimbia ovyo na kuanguka na watoto na kusababisha baadhi yao kuumia kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wanafunzi na baadhi ya viti kuvunjwa na wanafunzi hao, katika kurupushani hiyo baadhi ya wanafunzi walikamatwa na Polisi.

Katika Mahafali hayo ambayo baadaye yalifanyika chini ya ulinzi mkali baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi hao baada ya njia ya majadiliano kushindikana kutokana na jazba za wanafunzi hao waliokuwa walikuwa wakidai serikali ya wanafunzi ilirudishwe .

Hata hivyo Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina la Njechele Boniface alisema kuwa walianza kukusanyika chuoni hapo majira ya saa mbili asubuhi ili kufanya mkutano wao na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Deogratias Ntukumazina ili kuepuka kuingiliana na shughuli za mahafali hayo lakini Mwenyekiti wa Baraza la Chuo alifika chuoni hapo majira ya saa sita mchana na kusababisha kuingiliana kwa mkutano huo na shughuli za mahafali hayo.

Posted by Bigie on 7:35 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.