KIJANA MMOJA AUAWA KINYAMA USIKU HUU MKOANI IRINGA

Kijana akiwa hoi baada ya kucharangwa mapanga akituhumiwa kuiba Sinia katika moja kati ya vilabu vya pombe za Kienyeji eneo la Mshindo katika Manispaa ya Iringa
Hapa akiwa akiendelea kuvuja damu baada ya kipigo
Msamaria mwema akimtazama kijana huyo aliyetuhumiwa wizi akivuja damu
Hapa ndipo eneo la tukio
Polisi wakifika eneo la tukio
Polisi wakichukua mwili wa kijana huyo huyo baada ya kufariki dunia
WATU wanaodhaniwa kuwa na hasira kali wakazi wa Mshindo katika Manispaa ya Iringa wameumua kwa kumkata mapanga kijana mwenye miaka kati ya 25 na 30 mkazi wa Isoka mjini hapa wakimtuhumu kuiba sinia lenye chakula.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 usiku wa leo na mwili wa kijana huyo kukutwa katika klabu cha pombe za kienyeji cha Lebanon eneo la Mshindo huku sehemu za siri ukiwa umefunikwa kwa jacketi lake.
Mashuhuda waliozungumza na mtandao huu majira ya saa 7.20 za usiku baada ya kufika eneo la tukio walidai kuwa kinaja huyo alifika eneo hilo akiwa hoi na kueleza kilichomsibu kuwa alikuwa ameiba sinia lenye viazi na nyama kwa ajili ya kula na ndipo alipokutwa na mkasa huo wa kichapo.
Hata hivyo walisema baada ya kujipumzisha eneo hilo kwa zaidi ya saa moja bila kupata nafuu walinzi na wenyeji wa eneo hilo la klabu cha Lebanon waliamua kumzutia barabarani umbali wa hatua 16 na kumwacha hapo akinyeshewa na mvua kabla ya kufariki dunia.

Polisi walifika eneo hilo na kuuchukua mwili wake ,mwili uliokuwa na majeraha makubwa kichwani ,majeraha ambayo yanaonyesha wazi kuwa alikatwa na kitu chenye ncha kali kama panga ama kisu.
Mtandao huu  unalaani kwa nguvu zote uamuazi wa wananchi hao kujichukulia sheriamkononi dhidhi ya kijana huyo .Hata kama alikuwa mwizi hakupaswa kuuwawa na badala yake alipaswa kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Vitendo kama hivi vya wananchi kujigeuza mahakama na kutoa hukumu kama hizi zisifumbiwe macho hata kidogo .Ni vyema polisi kuwasaka wahusika ili sheria ichukue mkondo wake

Posted by Bigie on 6:48 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.