WATOTO WAFICHWA KIUCHAWI NA KUGEUZWA NDONDOCHA JIJINI DAR ES SALAAM
JAMII 10:34 PM
WIKI iliyopita, Ukonga -Mombasa eneo la Mongolandege, Dar kuliibuka tukio la kupotea katika mazingira tata, mtoto Mustafa Ramadhan (12), mwanafunzi wa Shule ya Msingi Gongolamboto, jijini Dar
Baada ya juhudi za wazazi kumtafuta mtoto huyo kushindikana, walikwenda kwa mganga maarufu jijini Dar, Jongo Salum ‘Manyaunyau’ ili awasaidie ‘kumtazama’ kwa tunguri alipo mtoto wao.
Baada ya juhudi za wazazi kumtafuta mtoto huyo kushindikana, walikwenda kwa mganga maarufu jijini Dar, Jongo Salum ‘Manyaunyau’ ili awasaidie ‘kumtazama’ kwa tunguri alipo mtoto wao.
Habari zinadai mganga huyo aliingia mzigoni kwa kutikisa vibuyu na ndumba za kila aina, mwishowe alibaini mtoto huyo alifichwa na wachawi kwenye Bonde la Mto Msimbazi, Dar akiwa hajitambui.
Wazazi sanjari na wanandugu wengine wakiwa na mganga huyo walikwenda hadi kwenye bonde hilo na kumpata mtoto Mustafa.
Wazazi sanjari na wanandugu wengine wakiwa na mganga huyo walikwenda hadi kwenye bonde hilo na kumpata mtoto Mustafa.
Akizungumza na Mpekuzi wetu baada ya zoezi hilo la kishirikina, Manyaunyau alisema:
“Kusema ukweli tabia za wachawi kuchukua watoto wa watu huku Ukonga Mombasa inazidi kushamiri, lakini juhudi za kukomesha tabia hii zinaendelea.”
Akiendelea kusimulia tukio hilo, Manyaunyau alisema mtoto Mustafa alipotea kwa siku ishirini huku kukiwa hakuna taarifa za mahali alipoonekana.
“Ni jambo la kusikitisha sana kwani mtoto mwenyewe tumemkuta ameshachanjwa ulimi na kutiwa madawa yao, hawezi kuongea. Walikuwa katika maandalizi ya kumfanya ndondocha wao, ila nakuahidi siku si nyingi ataanza kuongea vizuri,” alisema mganga huyo.