UZINDUZI WA ALBUM MPYA YA CHRITINA SHUSHO IITWAYO "NIPE MACHO" WASUBIRIWA KWA HAMU KUBWA....

WAIMBAJI wakali wa muziki wa Injili nchini, Upendo Nkone, Bahati Bukuku, Rose Muhando, Solomon Mukubwa na Bonny Mwaitege wanatarajiwa kumpa tafu mwenzao, Christina Shusho katika uzinduzi wa  albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Nipe Macho’.

Albamu hiyo itazinduliwa Desemba 23, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee kisha kuhamia katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar siku tatu baadaye.

“Diamond Jubilee kutakuwa na maombi ya nguvu kabla ya  uzinduzi utakaoanza saa 12 jioni mpaka saa 6 za usiku kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ambacho kitajumuisha na gharama za chakula, na Desemba 26, pale Leaders kiingilio kitakuwa ni Sh. 5,000 kwa wakubwa na Sh. 2,000 kwa watoto” alisema Shusho.

Posted by Bigie on 5:59 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.