"SIWEZI KURUDIANA NA H.BABA TENA"....FROLA MVUNGI
JAMII 12:39 AM
Siku chache baada ya kutosana na mchumba wake, Hamis Baba ‘H. Baba’, Flora Mvungi amedai hawezi kamwe kumrudia mwanaume huyo.
Akizungumza na Mpekuzi wetu hivi karibuni, Flora alisema kuwa anachukua uamuzi huo baada ya kuchoshwa na vipigo na manyanyaso ya H.Baba.
“Asikwambie mtu, pamoja na kwamba amenipigia magoti mpaka basi, lakini siwezi kurudi kwake ng’o. siyo yeye tu, hata ndugu zake wamenipigia simu, nikawaeleza mkasa mzima, wameniomba yaishe, lakini moyo wangu unakataa kufuatia maumivu niliyokuwa nayapata,” alisema Flora