"MIMI SI MGOMBANISHI ILA KUNA BAADHI YA WATU BONGO MOVIE NI WANAFIKI"....ZAMARADI
JAMII 12:39 AM
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Take One kupitia runinga
ya Clouds, Zamaradi Mketema amefunguka kuwa yeye si mgombanishi ila kuna watu Bongo Movie ni wanafiki.
ya Clouds, Zamaradi Mketema amefunguka kuwa yeye si mgombanishi ila kuna watu Bongo Movie ni wanafiki.
Akizungumza na Mpekuzi wetu hivi karibuni , Zamaradi alisema anashangaa kuambiwa anapoendesha kipindi chake huuliza maswali ya kimtego yenye lengo la kuwagombanisha wasanii.
“Jamani mgombanishi nitakuwa mimi? siwezi kufanya jambo hilo hata siku moja, wanaosema hivyo wana hila zao!” alisema Zamaradi.
Mtangazaji huyo aliamua kufunguka hayo kufuatia baadhi ya wasanii wa Bongo Movie kumcharukia kwa namna alivyolipalilia bifu la Irene Uwoya, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper.