LULU MICHAEL ASHEREHEKEA SIKUKUU "CHUMBANI"
JAMII 2:01 PM
STAA wa ‘picha’ za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema Sikukuu ya Krismasi alijifungia ndani kwa takribani saa 48, kuanzia siku ya mkesha na kesho yake, hali iliyomfanya mama yake mzazi kumshangaa.
Akizungumza na Mpekuzi wetu, kinda huyo mwenye akiba kubwa ya matukio, alisema kutotoka ndani hakujamtokea siku ya Krismasi tu, bali siku za karibuni amejikuta akiwa hivyo.
“Yaani jamani mi’ mwenyewe najishangaa, siku hizi sijui nini kimenitokea kwani nina muda mrefu sijapiga misele na naona kawaida tu,” alisema Lulu.
Aliongeza: “Mama mwenyewe alipata hofu akiamini naumwa, maana sikukuu nzima nishinde ndani mimi Lulu, wee.”