"UMAARUFU WANGU HUWAFANYA WANAUME WANIOGOPE"....ROSE CHITALA
JAMII 1:57 PM
Mtangazaji anayetumikia kituo namba moja cha redio Bongo, Times FM, Rose Bernad Chitala, amekiri baadhi ya wanaume kuogopa ‘kumtokea’ kutokana na umaarufu wake.
Akizungumza na Mpekuzi wetu jijini Dar es Salaam, juzi kuhusiana na maisha yake ya kimapenzi, Chitala alifunguka:
“Unajua umaarufu ni kazi sana, mtu anakuwa anakuogopa akidhani labda atakapokutokea utammwaga au anahisi huwezi kuwa na mapenzi ya kweli.”