"NATAMANI SANA KUFANYA KAZI NA DRAKE MAANA NI MSANII PEKEE ANAYEJITAMBUA"....AY
JAMII 6:59 PM
BAADA ya kurekodi ngoma kadhaa na wasanii kutoka Marekani Ambwene Yessaya ‘AY‘, amesema anatamani kufanya kazi nyingine na nyota wa kibao cha ‘Find your love’ (Drake) kwa kile alichodai kuwa ni msanii ambaye yuko katika chati za juu kwa sasa.
Alisema kuwa msanii huyo anauwezo mkubwa katika uimbaji hivyo anaamini endapo atapata nafasi ya kufanya naye ngoma itakuwa ni njia nzuri kwake ya kuweza kufikia malengo.
Alisema kuwa msanii huyo anauwezo mkubwa katika uimbaji hivyo anaamini endapo atapata nafasi ya kufanya naye ngoma itakuwa ni njia nzuri kwake ya kuweza kufikia malengo.

Aliongeza kuwa amemtaja nyota huyo kwani ndiye chaguo lake katika wasanii ambao anawazimia kutoka Marekani na ambao wanafanya kazi zinazopendwa zaidi duniani.
“Nampenda sana Drake, kwani ni msanii ambaye anajielewa hivyo naweza kufanya naye ngoma ingawa siyo leo kwa sababu kila kitu ni mipango pamoja na kumuomba Mungu,” aliongeza